BINGWA mara nane wa Olimpiki Usain
Bolt ameanza mazungumzo ya majaribio ya kusakata soka nchini Australia, klabu
moja imesema. Mwanariadha huyo wa jamaica, 31, anafanya mazungumzo ya kiusaini
kandarasi ya wiki sita n klabu ya Central Coast Mariners, klabu inayoshindana
katika ligi ya dara la A nchini humo.
Afisa Mkuu wa Klabu ya Mariners Shaun Mielekamp amesema kuwa
klabu hiyo ilitumia miezi minne kumsaka Bolt na mkataba wa muda mrefu huenda
ukafuata baadaye.
Bwana Rallis ambaye amehusika na mkataba huo aliambia Sky Sports
kwamba mazungumzo yanaendelea kuhusu mshahara wa Bolt.
''Mmiliki wa Central Coast Mariners ameamua kutafuta fedha zaidi
na kuhakikisha asilimia 70 ya mshahara wake'' , bwana Rallis alisema.
Chombo cha habari cha News Corp Australia kiliripoti kwamba
makubaliano ya mamilioni ya madola yameafikiwa.
Awali Bolt amekuwa akifanya mazoezi na klabu nchini Ujerumani ,
Norway na Afrika Kusini.
Bingwa huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mita 100 na 200
, ambaye alistaafu katika riadha mwaka uliopita amezungumzia kuhusu hamu yake
ya kutaka kucheza soka na kuwa mchezaji wa kulipwa.
Bolt ni shabiki wa Manchester United na naibu mkufunzi wa klabu
hiyo Mike Phelan sasa yuko katika klabu hiyo ya Mariners.
Shirikisho la soka nchini Australia limeambia BBC kwamba
halitahusika katika kufadhili majaribio ya Bolt. Bwana Mielekamp amesema kuwa
anatumai kwamba majaribio hayo yataongezewa muda.
''Iwapo kila kitu kitakuwa sawa, huwezi kujua? huenda akachezea
ligi ya daraja la A msimu huu, aliambia chombo cha habari chaSeven Network siku
ya Jumanne.
Bwana Mielkamp alisema kuwa klabu hiyo imepokea ripoti nzuri
kuhusu mchezo wa Bolt wakati alipofanya majaribio na klabu ya Ujerumani ya
Borussia Dortmund na timu ya Norway ya Stromsgodset.
"Kitu muhimu nadhani ni kusubiri kujua iwapo ni mchezaji
mzuri wa kiwango gani'', bwana Mielekamp alisema
"Wakati utasema yupo katika kiwango gani na iwapo anaweza
kucheza katika ligi ya daraja la A''.
No comments:
Post a Comment