RAIS MAGUFULI ATANGAZWA MSHINDI TUZO YA UKOMBOZI AFRIKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 17 July 2018

RAIS MAGUFULI ATANGAZWA MSHINDI TUZO YA UKOMBOZI AFRIKA

RAIS John Magufuli

RAIS wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrika katika masuala ya uchumi.
Makamo mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya ukombozi Afrika, Mwebesa Rwebugia ameieleza BBC kwamba rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana na mchango wake wa kiuchumi hasa katika ukuaji wa miundo mbinu.
Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa kuleta uhuru katika nchi za Afrika.
Mwebesa Rwebugia ameeleza kuwa, katika kuegemea kwenye muktadha wa uchumi, kamati iliangalia umaskini ambao unatajwa kuwa adui mkubwa anayefahamika, lakini pia maradhi na ujinga.
Kwa mujibu wa kamati hiyo ya Tuzo ya Ukombozi wa Afrika, ukombozi katika kipengelee cha elimu huangazia elimu na ujinga kama sehemu ya ukombozi.
Tanzania imetolewa mfano wa elimu ya bila malipo kutoka kutoka shule za
Katika suala la umaskini, kamati imeangalizia hatua ya kuwajali watu wa kipato cha chini, ukitolewa mfano wa kusajiliwa kwa 'machinga' katika kuwatambua rasmi kwa shughuli zao, na pia kuondolewa kodi za mazao kwa wananchi.
Lakini sio kila mtu amepokea vyema ushindi huu wa rais Magufuli kutokana na kwamba kiongozi huyo hajakamilisha hata miaka mitano tangu aingie madarakani.
Wakosoaji wanasema amepunguza nafasi ya raia kujieleze kwa uhuru.
Na serikali yake imekosolewa kwa hatua za kuvizima vyombo vya habari na kinachotajwa kama kuvikandamiza vyama vya upinzani.
'Rais magufuli hakutazamwa kwa muda aliyoingia madarakani lakini tangu miaka 20 iliyopita. Tangu alipokuwa wizara ya ujenzi na mawasiliano na nyingine tofauti, mpaka kufikia hadi ya kuwa rais wa taifa. Je ni mambo gani aliyoyafanya?' Amefafanua Rwebugia.
Mnamo 2016 Magufuli alishinda tuzo ya Forbes Africa kwa kuwa mtu anayeheshimika zaidi - na aliteuliwa kwa kutambulika jitihada zake za "kushinikiza uchumi wa Tanzania".
Tuzo ya Ukombozi Afrika inatambuliwa barani Afrika na Kimataifa lengo lake ni kutambua mchango wa viongozi wa bara la Afrika , wapigania uhuru, wapatanishi wa amani na washiriki wengine wa Ukombozi wa Afrika.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni mwishoni mwa mwaka jana aliwahi kuteuliwa mshindi na kamati inayoratibu Tuzo hiyo ya Ukombozi Afrika.


Ushindi wake Museveni ulitangazwa baada ya kamati hiyo kuketi mwezi Oktoba, 2017 na kujiridhisha kupitia vigezo vilivyowekwa kuwa kiongozi huyo anakidhi vigezo vyote.

No comments:

Post a Comment