Mkuu wa Wilaya ya Momba - Juma Irando akizungumza na
wafanyabiashara wa Mkoa wa Songwe ambao ni wanachama wa NMB Business Club
katika uzinduzi wa Business Club mpya uliofanyika mjini Tunduma juzi. Wengine
kwenye picha ni Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Straton Chilongola
(Kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha NMB – Donatus Richard.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha NMB – Donatus
Richard (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi
wa Business Club mpya uliofanyika mjini Tunduma juzi.
Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu – Straton Chilongola
akizungumza kwenye uzinduzi wa Business Club mpya uliofanyika mjini Tunduma
juzi.
Picha yapamoja kati ya mgeni rasmi paamoja na wakabidhiwa vyeti. |
NA MWANDISHI WETU
BANKI ya NMB imezindua rasmi
Klabu ya kibiashara maalumu kwa wafanyabiashara wa Tunduma katika wilaya ya Momba Mkoani
Songwe. Kuzinduliwa kwa Klabu hiyo ya Biashara kunafanya klabu za
biashara kuwa 35 nchini huku lengo lake likiwa ni kuwaunganisha wafanyabishara wa
kati na wakubwa na kuwa chombo cha kutatua changamoto zinazo
wakabili wafanyabiashara nchini.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara mjini
Tunduma juzi,
Mkuu wa Idara ya Biashara ya NMB – Donatus Richard alisema kuwa
benki hiyo
imedhamiria kurahisisha huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali
hususani
wafanyabiashara ambao ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini.
Bwana Donatus alisema kuwa ili kuhakikisha benki inachangia
ukuaji wa sekta ya
biashara nchini, imeanzisha vilabu vya wafanyabiashara (NMB
Business Clubs) ili
kukuza na kuimarisha biashara nchini.
Alisema kuwa NMB Business Club zina malengo ya kuifikia jamii
ya
wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa ambao
wanajumuisha
wafanyabiashara wateja wa NMB zaidi ya 50,000 nchi nzima huku
biashara yao
ikifikia thamani ya shilingi bilioni 600. NMB Business Club ni
mahali muafaka pa
kuelimisha wafanyabiashara juu ya masuala mbalimbali kuhusu
biashara zao.
“Ndugu Mkuu wa Wilaya, Lengo la kuanzisha NMB Business Club ni
kuhakikisha
wafanyabiashara hawa wanakuza mitaji yao, kuajiri watanzania
wengi zaidi na pia
kuchangia uchumi wa taifa hili kupitia ulipaji kodi.” Alisema
Donatus.
Donatus aliongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa NMB Busines Club,
wanachama
wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya
kutumia vitabu
vya mahesabu, elimu ya masoko na pia elimu ya mlipa kodi kwa
kushirikiana na
mamlaka ya mapato nchini TRA.
Aidha katika hatua nyingine Donatus alisema Jumla ya Club 35
zime anzishwa
na wanachama 20000 wameshanufaika na huduma zinazotolewa na NMB
huku
akieleza kuwa Mpango wa Bank ni kufikia wanachama 25000 ifikapo
mwishoni
mwa mwaka 2018.
“Nmb Business Club zina malengo ya kuifikia jamii ya
wafanyabiashara wadogo
na wa kati. Kwa sasa, Nmb Bank inahudumia wafanyabiashara zaidi
ya 200,000
ambao ni wateja nchi nzima ambapo wana mikopo ya biashara yenye
dhamni ya
zaidi ya bilioni 600,” alisema Donatus.
Naye Mkuu wa Wilaya ya hiyo Juma Irando ambaye alikuwa mgeni
rasimi kwenye
hafla ya ufunguzi wa Busines Club alipongeza bank hiyo kwa
kuamua kutoa elimu
ya mlipakodi, utunzaji wa kumbukumbu na pia jinsi ya kuweka
mahesabu sawa.
“Niipongeze Nmb kwa kutoa mafunzio haya kwani moja ya eno ambalo
wafanyabiashara wengi wanakosa ni hili la Ulipaji kodi na
utunzaji wa
kumbukumbu hivyo niimani yangu kuwa litapunguza sana migogoro
kati ya
wafanyabisha na Serikali hasa TRA,” alisema Irando.
No comments:
Post a Comment