Kushoto ni Mkurugenzi wa Redio Habari Maalumu, akijitetea mbele ya viongozi wa TAMUFO.
Viongozi wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Kwaya mbalimbali na Uongozi wa Redio Habari Maalumu wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya matumizi ya kazi zao. Kulia ni Rais wa TAMUFO, Dk.Kisanga na nyuma yake ni Katibu wa TAMUFO, Stellah Joel.
Mwenyekiti wa Kwaya za Ulyankulu aliyeshika faili akieleza jinsi nyimbo zao zinavyotumika mitandaoni pasipo kunufaika nazo.
Picha ya pamoja baada ya mkutano huo. Wa tatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel na wa pili ni Mkurugenzi wa Redio Habari Maalumu.
Viongozi wa TAMUFO, Dk.Donald Kisanga na Katibu wake, Stellah Joel, studio ya Arusha One Redio kuhakikisha wanamuziki wa Kanda ya Kaskazini wanapata elimu ya kunufaika na kazi zao za sanaa kwani TAMUFO ni mkombozi wa wasanii
Na Dotto Mwaibale
UMOJA wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) umetoa onyo kali kwa Redio Habari Maalumu Kuhakikisha haisambazi nyimbo za wasanii bila kufuata utaratibu halali.
Onyo hilo limetolewa na Rais wa TAMUFO Dk. Donald Kisanga katika mkutano uliowakutanisha TAMUFO na vionozi wa redio hiyo pamoja na wadau wengine.
"Baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa Kwaya kongwe hapa nchini kuhusu kazi zao kutumiwa na redio hilo bila faida tuliamua kufanya ziara ya kikazi jijini Arusha kwa ajili yakuja kuyatafutia ufumbuzi malalamiko hayo na kuongea na wahusika" alisema Kisanga.
Kisanga alizitaja kwaya zilizotoa malalamiko kuwa ni Ulyankulu Mapigano na Ulyankulu Barabara ya 13 zote za Tabora na Kwaya Kuu Habari Njema Kwaya ya Uinjilist za Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mjini kati zote za Mkoani Arusha.
Alisema TAMUFO baada ya kupokea malalamiko hayo iliweza kuwakutanisha Vikundi hivyo vya kwaya Pamoja na redio hiyo na kumaliza mgogoro huo ambapo walifikia muafaka kwa makubaliano kwa Kwaya husika iliitaka redio hiyo iwalipe gharama za usumbufu.
Baada ya Makubaliano hayo Dk. Kisanga aliwaonya Redio Habari Maalum kuacha mara moja kuendelea kuuza kazi za Wanakwaya pasipo kuwa na mkataba.
Viongozi wa TAMUFO bado wapo katika ziara ya kikazi mikoa ya Kanda ya Kaskazini kukutana na wadau wa muziki wa injili ili kujua changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment