NAIBU Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko amewataka wazazi na walezi Nchini kuhakikisha wanalea watoto wao katika misingi iliyo bora ili kupata Taifa bora na viongozi bora wa kesho huku akiipongeza benki ya NMB kwa kushirikiana na serikali kuboresha sekta ya elimu Nchini.
Alisema kuwa iwapo watalelewa katika mazingira ya ukatili, unyanyasaji na kukatishwa tamaa ndio kunakozalisha viongozi wakatili wa baadae.
Naibu Waziri Mkuu Biteko ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya mtoto wa leo Samia wa kesho inayokwenda sambamba na juma la elimu iliyofanyika Wilayani Muheza Mkoani Tanga.
“Niwatake wazazi,walezi na walimu kushirikiana katika jkuwasomesha watoto vizuri ili waweze kupata Samia wa kesho au viongozi waliobora kwani mwalimu akitimiza wajibu wake na mzazi akitimiza wajibu wake ndio tutakapozalisha kijana atakayekuwa na mchango mzuri kwa jamii,” alilisitiza Dkt. Biteko.
Aidha alisema pamoja na mazingira ya kielimu yaliyopo Nchini Jukumu la kuzalisha wanafunzi waliobora lipo mikononi mwa walimu ambao wanajumuku la kutengeza Taifa la kesho la watu wenye kufuata mila na desturi zilizobora.
Dkt. Biteko amesema kwamba kampeni hiyo imejengwa kwenye misingi ya utatu katika kuhakikisha mtoto anapata elimu bora kwa ushiriki wa wazazi, serikali na wadau ikiwemo benki ya NMB ili kuboresha mazingira ya kielimu kwa wanafunzi hapa nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema kuwa kongamanio hilo nisehemu ya jitihada ya kuinua kiwango cha elimu ikiwemo na kutatua changamoto zilizopo.
Balozi Dkt Batilda amesema kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo katika sekta ya elimu Mkoani humo ni kiwango cha ufaulu kutoridhisha katika shule za msingi ni asilimia 74.4 huku kwa upande wa sekondari ikiwa ni asilimia 89.
“Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NMB tunakwenda kurudisha Mkoa wa Tanga kwenye ramani ya kieleimu hususani wilaya hii ya Muheza,” alisisitiza Balozi Dkt. Batilda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa juma la elimu ‘Mtoto wa leo Samia wa kesho’ Afisa Mkuu wa Udhibiti benki ya NMB Doreen Joseph amesema katika kuunga mkono juhudi za serikali benki hiyo imetoa msaada wa vifaa venye thamani ya shilingi Mil 60 kwa ajili ya shule tano za msingi ziliozopo wilayani humo.
“Katika kurudisha kwa jamii tumejikita katika kutatua changamoto za sekta ya elimu nchini ni kipaumbele kwetu hii ni kutokana kutambua juhudi za Serikali ya kusimamia elimu hivyo tumeona tutoe msaada huo,“ alisema Joseph.
“Pamoja na makubwa yote ambayo serikali yetu inaendelea kuyafanya, sisi kama wadau ni furaha kwetu kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii yetu kwani ni jamii hii iliyoiwezesha benki ya NMB kuwa hapa ilipo na kuwa benki yenye maendeleo kuliko benki yoyote hapa nchini kwa hili naomba kuwashukuru sana,”alisema.
“Mheshimiwa Mgeni rasmi ni faraja kwa benki yetu ya NMB kushirikiana na serikali katika kuboresha mazingira ya elimu katika wilaya hii ya Muheza kwa kuchangia vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 60 ili kutatua changamoto mbalimbali,”
Aidha alivitaja vifaa hivyo kuwa ni Madawati 200 kwa ajili ya Shule za Msingi za Kwemkabala, Masuguru,Mdote, Mwembeni na Ngomeni na kila shule itapata madawati 50 lakini pia tumetoa Vitanda 40 na magodoro 80 kwa ajili ya Shule ya Msingi Ngomeni vitanda 32 na magodoro 64 kwa ajili ya Shule ya Msingi Masuguru.
Naibu waziri wa elimu,sayansi na teknolojia Omari Kipanga amesema kongamano hilo limelenga kushirikisha wadau wa elimu katika kuunga mkono jitihada zaserikali katika kuboresha mazingira ya elimu na kuwasaidia watoto waweze kukosa sehemu nzuri.
No comments:
Post a Comment