NMB YACHANGIA MILIONI 50 UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA BUNGE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 4 September 2024

NMB YACHANGIA MILIONI 50 UJENZI SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA BUNGE
















Na Mwandishi Wetu, Dodoma

BENKI ya NMB imekabidhi Hundi ya Shilingi milioni 50 kwa Naibu Waziri Mkuu Dk Dotto Biteko kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Wavulana ya Bunge. Wakati wa Bonanza la Bunge, NMB pamoja na wadau wengine katika viwanja vya shule ya sekondari John Merlin Jijini Dodoma.

Naibu Waziri Dk Biteko amepokea Hundi hiyo na kusema itasaidia kuwapa nguvu wabunge katika safari ya ujenzi wa shule hiyo baada ya kukamilika kwa shule ya Wasichana ya Bunge.

Dk Biteko ameipongeza benki hiyo kwa namna inavyokuwa karibu na Watanzania katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo kwenye michezo kama ilivyofanyika katika Bonanza hilo la NMB Bunge Bonanza ambalo benki hiyo ilichangia vifaa mbalimbali na vitu vingine.

“Nawapongeza NMB kwa kujinyima na kutoa sehemu ya mapato yenu, msiache kutushika mkono wakati mwingine tukiwahitaji, niwaombe na wadau wengine kwa ajili ya kuunga mkono ujenzi wa shule hiyo muhimu kwa ajili ya vijana wetu,” amesema Dk Biteko.

Akizungumzai Kauli mbiu ya Tamasha hilo kuhusu Ushiriki wa Uchaguzi, Naibu Waziri amewaomba Watanzania kutokuchukulia poa kwani Serikali inaanzia vitongojini kabla ya kufika kwenye ngazi ya Taifa.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Juma Kimori ndiye aliye kabidhi hundi hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ambaye alikuwa yuko nje ya nchi kwa majukumu mengine.

Kimori amesema benki hiyo itaendelea kutoa michango yake kwa jamii kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita pamoja na kazi mbalimbali zinazofanywa na wabunge kuanzia majimboni mwao.

“Tumekuwa tukiunga mkono kwenye masuala ya Afya, Elimu na majanga, tutaendelea kushirikiana katika kupeleka maendeleo kwa wananchi na ndiyo maana tumefika katika kila wilaya lakini tunalenga kumfikia kila Mtanzania,” amesema Kimori.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Mhe. Dk Tulia Akson amesema NMB imekuwa karibu na bunge wakati wote na kila wanapowaomba wamekuwa wakiwaunga mkono lakini hata kwenye majimbo ya mtu mmoja mmoja nako wanafanya hivyo.

Dk Tulia amesisitiza umuhimu wa kushirikiana  na NMB katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili lakini matumizi sahihi ya benki kwa watu wa ngazi zote ikiwemo waishio vijijini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Mhe. Festo Sanga amesema mbali na kudhamini Bonanza hilo, lakini NMB wameonyesha ushindani mkubwa hata kuishinda Timu ngumu ya Bunge ya Mpira wa Miguu kwa magoli 3-0.

Sanga amesema ushiriki wa michezo kwa Watanzania unasaidia kujenga afya na kupunguza gharama ambazo zingetumika kwa ajili ya kuwatibu na kuwajengea afya na kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa.

No comments:

Post a Comment