DKT. NCHEMBA ZIARANI OMAN APONGEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 17 December 2024

DKT. NCHEMBA ZIARANI OMAN APONGEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI

 

Kamishna wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Bw. Johnson Nyella, akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab, mazungumzo yaliyofanyika katika Makazi yake mjini Muscat-Oman. 

Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Robert Mtengule, akichangia mada wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab na watumishi wa Ubalozi huo na wadau wengine. Kushoto ni Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Wizara ya Fedha, Bw. Elias Kimati.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kulia) akiongoza kikao alipoongoza Ujumbe wa Tanzania katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mheshimiwa Fatma Rajab. 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Oman Mheshimiwa Fatma Rajab, akizungumza wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi huo, katika Makazi yake, Mjini Muscat-Oman. Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, yuko katika ziara ya kikazi nchini humo.

No comments:

Post a Comment