CHAGUENI VIONGOZI WAADILIFU-PINDA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 27 September 2024

CHAGUENI VIONGOZI WAADILIFU-PINDA

Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati wa Kikao cha Halmashauri ya CCM kata ya Majimoto wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 26 septemba 2024 katika Shule ya Msingi Majimoto.

Sehemu ya wana CCM wakiwa katika kikao cha Halmashauri ya CCM kata ya Majimoto wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi tarehe 26 septemba 2024 katika Shule ya Msingi Majimoto.

Na Mwandishi Wetu, MLELE

MBUNGE wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. Geophrey Pinda amewataka wananchi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchagua viongozi waadilifu ambao hawataiingiza jamii kwenye matatizo yakiwemo yale ya sekta ya Ardhi. 

 

Mhe Pinda amesema hayo katika Kikao cha Halmashauri ya CCM kata ya Majimoto wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi kilichofanyika jana katika Shule ya Msingi Majimoto.

 

Amewaeleza wajumbe wa mkutano huo namna ambayo Wenyeviti wa Mitaa wanavyochangia migogoro ya ardhi jambo alilolieleza kuwa limetokana na kufanyika makosa wakati wa kuwachagua viongozi hao.

 

"Huko Wizara ya Ardhi, jamani migogoro mingi ni ya wenyeviti kuuza maeneo bila ridhaa ya wananchi " amesema mhe. Pinda

 

"Sasa tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ombi langu tukawapitishe watu kama mlivyonipitisha mimi na mimi nilivyowapitisha nyie kwa sifa zenu" amesongeza mhe. Pinda.

 

Kwa mujibu wa Mbunge huyo wa jimbo la Kavuu, kiongozi bora ni yule aliye tayari kujitolea kwa moyo Kufanya kazi kizalendo kwa ajili ya wananchi wote nchini.

 

Mhe. Pinda amebainisha kuwa, kutokana na utendaji bora unaofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haoni kama kuna nafasi ya vyama vya upinzani  kusimamisha mgombea.

 

Mhe. Geophrey Pinda yupo katika ziara jimboni kwake ambapo mbali na mambo mengine  anatembelea kata zote ndani ya jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment