SERIKALI YASITISHA ZOEZI LA UKAGUZI WA RISITI SOKO LA KARIAKOO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 24 June 2024

SERIKALI YASITISHA ZOEZI LA UKAGUZI WA RISITI SOKO LA KARIAKOO

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa pili kushoto) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakizungumza na Viongozi wa wafanyabiashara baada ya kumalizika kwa kikao kati yao jijini Dodoma, ambapo Serikali imeridhia kusitisha zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, wakati ukiandaliwa utaratibu mzuri wa utekelezaji wa suala hilo katika Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Bw. Martin Mbwana, akieleza changamaoto mbaoimbali za wafanyabiashara wa Soko hilo ikiwemo ya zoezi la ukaguzi wa risiti za Kielekroniki (EFD) na ritani za kodi (VAT), iliyokuwa ikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia mkoa wa kikodi wa Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, ambalo Serikali imelisitisha, wakati wa mazungumzo kati ya Wafanyabiashara na Serikali, jijini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Felesh, akieleza umuhimu wa wafanyabiashara nchini na namba ambavyo inashughulikia na kurekebisha sheria mbalimbali za masuala ya kodi, wakati wa kikao kati ya Viongozi wa Wafanyabiashara Tanzania, Viongozi wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo na Taasisi zinazosimamia masuala ya wafanyabiashara, kikao ambacho kiliitishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment