BASHUNGWA AZIKUTANISHA TEMESA NA AZAM MARINE UBORESHAJI HUDUMA ZA VIVUKO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 10 May 2024

BASHUNGWA AZIKUTANISHA TEMESA NA AZAM MARINE UBORESHAJI HUDUMA ZA VIVUKO

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akifafanua jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Katibu Mkuu wa Ujenzi, Balozi Mhandisi Aisha Amour, timu ya watalaam kutoka TEMESA na uongozi wa Azam Marine (hawapo pichani), kujadili namna ya kuendelea kushirikiana kwa pamoja kuboresha utoaji wa huduma za usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni – Kigamboni jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Azam Marine, Abubakar Aziz akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa katika kikao kazi kilichowakutanisha timu ya watalaam kutoka TEMESA na uongozi wa Azam Marine katika kikao kikazi cha kujadili namna ya kuendelea kushirikiana kwa pamoja kuboresha utoaji wa huduma za usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni – Kigamboni jijini Dar es Salaam.


Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Ujenzi wa Vivuko kutoka TEMESA, Eng. Sylvester Simfukwe akifafanua jambo katika kikao kazi kilichokutanisha uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Timu ya watalaam kutoka TEMESA na uongozi wa Azam Marine kujadili namna ya kuendelea kushirikiana kwa pamoja kuboresha utoaji wa huduma za usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni – Kigamboni jijini Dar es Salaam

 

No comments:

Post a Comment