TUATAENDELEA KUIHIMARISHA TTCL KUCHANGIA UCHUMI WA KIDIJITALI - WAZIRI NAPE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 9 July 2023

TUATAENDELEA KUIHIMARISHA TTCL KUCHANGIA UCHUMI WA KIDIJITALI - WAZIRI NAPE

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kulia) alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga (wa tatu kushoto) wakifurahiya jambo wakati Waziri huyo alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushotyo mwenye miwani ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga akiambatana naye. 

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga (wa kwanza kulia) akimuonesha kumbukumbu ya historia ya mawasiliano ya simu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (wa tatu kulia) pamoja na viongozi alioambatana nao katika picha ya kumbukumbu alipotembelea Banda la TTCL kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa. Wa kwanza kulia ni mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga.

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amesema Serikali inaendelea kulihimarisha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) pamoja na taasisi zingine zitakazochangia ukuaji na kujenga uchumi wa kidigitali nchini.

Waziri Nnauye aliyasema hayo kwenye Viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa akizungumza katika Kongamano la TEHAMA Ukumbi wa Sabasaba Expo Village, pamoja na kutembelea Banda la TTCL lililopambwa na historia ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania.

Alisema Serikali kupitia wizara yake imelihimarisha Shirika la TTCL ikiwemo kuwakabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data kimtandao 'Data Center' na Mungu akipenda wataikabidhi pia Setelite ili kuhakikisha taifa linajenga uchumi wa kidigitali.

Wizara imepewa jukumu la kujenga uchumi wa kidigitali, hivyo inaendelea kuihimarisha TCRA, imeunda pia tume ya Tehama, hii yote ni kuendelea kujenga miundombinu bora ya taasisi ambayo itasimamia na kujenga uchumi wa  kidigitali.

Aidha alisema Serikali ipo kwenye mapitio ya sera, kanuni na sheria ili kuwa na mfumo bora wa kidigitali ambao utaondoa utapeli, rushwa na kuvutia wawekezaji.

Alisema maonesho ya Sabasaba kwa mwaka 2024 kutakuwa na maboresho makubwa kiteknolojia kwani watakaoudhuria hawataangaika tena kutafuta mabanda ya taasisi au maduka yanayoshiriki kwenye maonesho kwa kuwa utafungwa mfumo maalum sehemu za kuingilia watu ambao utamuonyesha muhusika njia na eneo analotaka kutembelea.

“Tunataka watu wa kidigitali tuyateke maonesho haya, naamini inawezekana na nitasimamia hili, na ninataka nione mapendekezo namna maonesho yajayo yatakavyokuwa bora zaidi,” alisema Waziri huyo mwenye dhamana ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nnauye.

No comments:

Post a Comment