NBC YAZINDUA KAMPENI YA FUNGA MWAKA KIBABE NA NBC - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 5 December 2022

NBC YAZINDUA KAMPENI YA FUNGA MWAKA KIBABE NA NBC

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias (katikati) ,Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kibenki ya kidijitali inayoitwa "Funga Mwaka Kibabe na NBC Bank." Kampeni hii inalenga kukuza matumizi ya chaneli za kidijitali mtandaoni kwa wateja wa Benki ya NBC wakati wa msimu wa sikukuu.Pembeni kulia yake ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha masoko David Raymond na maafisa wengine wa Benki hiyo wakishuhudia uzinduzi huo.Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni wa wiki iliyopita Jijini Dar es salaam.
  • Benki ya NBC yazindua kampeni ya kibenki ya kidijitali kuzawadia zaidi ya wateja 400
KATIKA juhudi za kukuza miamala ya papo kwa papo, salama na malipo ya bila kutumia pesa taslimu nchini, Benki ya NBC imezindua kampeni yake mpya ya kibenki ya kidijitali inayoitwa "Funga Mwaka Kibabe na NBC Bank." Kampeni hii inalenga kukuza matumizi ya chaneli za kidijitali mtandaoni kwa wateja wa Benki ya NBC wakati wa msimu wa sikukuu. Mapinduzi mapya ya malipo yanayofanyika kupitia viza ( Visa) yatawahakikishia usalama wateja na urahisi zaidi wa kufanya malipo. 

Katika jitihada za kukuza miamala salama na ya papo kwa papo isiyotumia nguvu nyingi, na malipo ya bila kutumia pesa taslim nchini! Kupitia kampeni hii mpya, wateja wa Benki ya NBC wanaofanya miamala kupitia njia mbadala za kidijitali za NBC Kiganjani,huduma ya benki kupitia mtandao na kupitia kadi ya NBC Debit watapata fursa ya kujishindia zawadi za pesa taslimu, simu za mkononi, luninga na mengine mengi. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias, alisema kampeni hiyo mpya inalenga kuhakikisha wateja wanaweza kupata pesa zao kwa usalama na kufanya miamala kwa urahisi, kuongeza urahisi zaidi wa huduma na kuboresha uzoefu kwa wateja. 

“Tunataka kuwapa wateja wetu muda wa kutosha kwa ajili ya familia na wapendwa wetu katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwahakikishia kwamba wanaweza kufanya miamala yote ya benki wakiwa katika hali ya starehe wakiwa majumbani mwao. Tunaelewa kuwa wengi watakuwa likizoni na pengine kujiingiza katika matembezi mengi ya matumizi katika wakati huu. Benki ya NBC imehakikisha kuwa unaweza kufanya miamala kwa urahisi na kwa ufanisi ukiwa nyumbani huku ukipata nafasi ya kujishindia zawadi”. Alisema Ulrik.   

 Ulrik pia aliongeza kuwa kampeni hiyo inalenga kuwazawadia watumiaji. Kadiri unavyofanya miamala mingi, ndivyo unavyojishindia na kupokea zawadi za kampeni kama vile simu za mkononi, luninga, punguzo la asilimia 40 kwa ununuzi mbalimbali, zawadi za pesa taslimu na vocha za kufanyia manunuzi.

  “Wateja wote wanaotumia kadi zetu za benki za visa, ATM, App ya NBC ya simu, na huduma za NBC Kiganjani watakuwa na nafasi sawa za kushinda zawadi hizi. Wanachotakiwa kufanya ni kufanya miamala. Kutakuwa na droo za kila wiki, droo za kila mwezi, na zawadi za papo hapo zitashindaniwa. Tunalenga kuwazawadia zaidi ya wateja 400 waaminifu. Tutahakikisha kuwa kuna miamala isiyo na matatizo katika msimu huu wa sikukuu ili wateja wetu waweze kufurahia na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kwa kutumia chaneli za kibenki za kidijitali.” Alisema Ulrik. 

Kampeni itaanza tarehe 2 Desemba 2022 hadi Januari 26, 2023. Benki imeshirikiana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ili kuhakikisha kwamba ushindi wote ni wa haki na wa wazi. Washindi watatangazwa na kutunukiwa hadharani. 

  Funga mwaka Kibabe ni mpango wa NBC unaolenga kuboresha uzoefu wa kibenki wa kidijitali kwa wateja kupitia chaneli mbalimbali. Kampeni hii inajikita katika kutoa suluhisho za kufanya miamala kidigitali ambapo pia wateja wanapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali haswa msimu huu wa sikukuu. Zawadi zitapatikana kupitia droo za bahati nasibu za kila wiki na kila mwezi ambapo wateja lazima wawe wamefanya miamala zaidi ya mara 20 hadi 70 ili kuboresha nafasi zao za kushinda.

No comments:

Post a Comment