Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe akiwasilisha mada ya kuwajengea uelewa juu ya Elimu ya Usalama Mtandao Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha jana Oktoba 17, 2022.
Elimu ya usalama mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha ikitolewa.
Mtaalam wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Kidijitali, Bw. Yusuph Kileo akiwasilisha mada ya kuwajengea uelewa juu ya Elimu ya Usalama Mtandao Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha jana Oktoba 17, 2022.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mafunzo ya elimu ya Usalama Mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha.Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe (kulia) akimkabidhi tshirt Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dkt. Cairo P. Mwaitete mara baada ya semina ya Usalama Mtandao kwa wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiko jana Oktoba 17, 2022, jijini Arusha.
Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mafunzo hayo.Mafunzo yakiendelea.
Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe (kulia) akimkabidhi tshirt Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Dkt. Cairo P. Mwaitete mara baada ya semina ya Usalama Mtandao kwa wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiko jana Oktoba 17, 2022, jijini Arusha.
Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha
WATUMISHI wa umma na binafsi wametakiwa kuwa makini na chochote
wanachofanya mtandaoni ili kujilinda na changamoto za uhalifu wa mtandao ambapo
katika zama hizi za kidijiti taarifa binafsi au za taasisi zimegeuka kuwa
malighafi muhimu kwa wahalifu wa mtandao.
Vifaa na mifumo ya TEHAMA ambayo hutumika kupitisha taarifa binafsi au za
taasisi vimekuwa vikishambuliwa zaidi na wahalifu kwa njia mbalimbali lengo
likiwa ni kupata taarifa za kibenki, nywila n.k.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara ya
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Stephen Wangwe wakati
akitoa elimu ya usalama mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha jana Oktoba 17, 2022, jijini Arusha.
Mhandisi Wangwe amesema kuwa suala la usalama mtandao ni changamoto ya
kidunia ambapo takwimu zinaonesha kila siku majaribio milioni 156 ya uhalifu
kwa njia ya barua pepe au tovuti hutokea na majaribio milioni 16 hufanikiwa.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo imeendelea kuimarisha usalama
wa mtandao kwa kujenga mazingira wezeshi na mifumo imara ya kusimamia sera,
sheria, kanuni na miongozo ya usalama wa mtandao pamoja na kutoa elimu kwa
makundi yote katika jamii ili kupunguza mianya ya uhalifu wa mtandaoni.
“Usalama wa mtandao huanza na mtu binafsi, pamoja na juhudi nyingi
zinazofanywa na Serikali, bado kila mtu analo jukumu la kuchukua tahadhari na
kujilinda na uhalifu unaofanywa kwa njia ya mtandao”, Amesema Wangwe.
Naye Mtaalamu wa Masuala ya Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Kidijiti wa
African ICT Alliance (AfICTA) kutoka Tanzania, Bw. Yusuph Kileo amesema kuwa,
namba ya siri imara na madhubuti ni kitu cha kwanza na cha msingi za kujilinda
na uhalifu wa mtandao lakini pia umakini na kuchukua tahadhari kutawaepusha
watumiaji kuwa wahanga wa uhalifu wa mtandao.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Wangwe amewataka wanafunzi wa Chuo cha
Uhasibu cha Arusha (IAA) kutafakari mara mbili kabla ya kuweka chochote
mtandaoni ili kujiepusha na matukio ya udhalilishaji na utapeli ambayo yanaweza
kuathiri maisha yao ya baadae.
Akijibu maswali mbalimbali ya wanafunzi chuoni hap oleo oktoba 17, Mhandisi
Wangwe ametolea ufafanuzi masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na huduma ya bure ya
kutafuta simu iliyoibiwa na umakini wa Serikali wa kujiridhisha kabla ya
kuzifungia namba za simu zilizoripotiwa kufanya uhalifu kupitia namba 15040.
Mapokeo ya Elimu ya Usalama mtandao kwa Menejimenti ya Chuo cha Ufundi cha Arusha na wanafunzi wa Chuo cha IAA yamekuwa ni mapokeo chanya ambapo kwa nyakati tofauti wamekiri kuwa elimu iliyotolea imewafungua katika maeneo mengi sana na matamanio yao ni Wizara kuendelea kutoa mafunzo haya mara kwa mara na kuyafikia makundi yote ya kijamii.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
No comments:
Post a Comment