MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariamu Mwinyi ameishukuru Jumuiya Health Rockfeller Foundation kutoka nchini Marekani kwa azma yake za kusaidia juhudi za Serikali katika kujikinga na Ugonjwa wa Covid -19.
Mama Mariamu ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) ametoa shukurani hizo Ikulu Migombani mara baada ya mazungumzo na Ujumbe wa Jumuiya Health Rockfeller Foundation ulioongozwa na Makamo wa Rais Andrew Sweet, ambapo Jumuiya hiyo itasaidia Progamu ya utoaji wa chanjo za Ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini.
Amesema ZMBF inathamin juhudi za Jumuiya hiyo kwa vile inayolenga kuimarisha afya za wananchi katika kujikinga na ugonjwa huo.
Alisema mradi huo ni wa mwaka mmoja itatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya hizo mbili, AMREF pamoja na Wizara ya Afya katika Wilaya za Magharibi ‘A’ pamoja Kaskazini ‘A’ Unguja.
Nae, Makamo wa Rais wa Jumuiya ya Health Rockfeller Foundation Andrew Sweet alisema ni jambo la faraja kwa Jumuiya hiyo kuwa na ushirikiano na ZMBF na kupata fursa ya kuwasaidia huduma za chanjo ili wananchi waweze kukabiliana na ugonjwa Covid -19
Aidha, Mjumbe wa Bodi ya ZMBF Dk. Ellen Mkondya Senkoro alisema Programu inayolengwa kutekelezwa ni kubwa na kubainisha matumaini yake kuwa mradi huo utatowa matokeo chanya
No comments:
Post a Comment