SERIKALI ya Tanzania imeahidi kushirikiana na nchi ya Uturuki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini ikiwemo Ujenzi wa Chelezo na Meli katika Ziwa Tanganyika.
Akizungumza na Mjini Ankara Nchini Uturuki Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kukutana na Waziri Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki Adil Karaismailogly Jijini Ankara - Uturuki amesema utekelezaji mzuri wa mradi wa reli ya Kisasa ya SGR kupitia kampuni YEPMAREKZ nchi hiyo umechangia kufaya mazungumzo ili kuona maeneo mbalimbali ya ushirikiao.
“Kampuni ya Yapi Merkezi ni ya nchini uturuki na wanatekeleza mradi wa Reli yetu nchini kwa awamu zaidi ya mbili hii imetupa hamasa ya kuzungumza nao ili kuona uwezekano wa wao kupata miradi mingine inayotekelezwa na Serikali,” Amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof Mbarawa amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi yote iliyopanga kwa mwaka wa fedha 2022/2023 hasa ile iliyopangwa kutekelezwa katika Ziwa Tanganyika kwa kujenga meli kubwa lengo likiwa ni kuboresha usafiri na usafirishaji nchini na hivyo kuchochea uchumi wa Taifa.
Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa meli iliyopangwa kujengwa katika Ziwa Tanganyika inatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba tani elfu tatu, meli ya kubeba Makasha, meli ya abiria 600 pamoja na mizigo tan 400 pamoja na chelezo chenye uwezo wa chenye uwezo wa kubabeba meli yenye tan elfu tano.
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki Adil Karaismailogy amesema kuwa Serikali ya Uturuki iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kupata makampuni mazuri ya ujenzi wa Meli, Vivuko na chelezo.
Waziri Prof. Mbarawa yuko nchini uturuki kwa ziara ya siku 5 ya kuzungumza na wawekezaji mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu nchini.
No comments:
Post a Comment