DKT MABULA ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA SHELTER AFRIQUE VICTORIA FALLS ZIMBABWE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 27 July 2022

DKT MABULA ASHIRIKI MKUTANO MKUU WA SHELTER AFRIQUE VICTORIA FALLS ZIMBABWE

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akishiriki Mkutano Mkuu wa 41 wa mwaka wa Taasisi ya Shelter Afrique unaoendelea katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe jana.

Na Munir Shemweta

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula anahudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 41 wa Taasisis ya Shelter Afrique unaoendelea katika mji wa Victoria Falls Magharibi mwa Zimbabwe.

Tanzania ni mwanachama wa Taasisi ya Shelter Afrique na inahudhuria mkutano huo kwa kuwa ina haki ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya taasisi hiyo.

Shelter Afrique ni Taasisi ya fedha inayoundwa na serikali za nchi za Afrika kwa kushirikiana na Benki ya Afrika ambazo zinachangia mtaji kwa kununua hisa na kujenga mtaji unaotumia na nchi wanachama katika shughuli za maendeleo ya nyumba na miji kwenye Bara la Afrika.

Kauli mbiu ya mkutano huo unaotarajiwa kumalizika tarehe 29 Julai 2022 ni ''Climate Change and the Built Environment'' ambapo Tanzania kwenye mkutano huo inawakilishwa na Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Uendelezaji Milki  Lucy Kabyemela.

Mkutano mkuu wa 41 wa mwaka wa Taasisi ya Shelter Afrique ni moja ya shughuli muhimu za taasisi hiyo katika mikakati yake ya kipindi cha mwaka 2020- 2025. 

No comments:

Post a Comment