Kanali Kinana akielekea eneo la mradi huo kwa ajili ya kukagua maendeleo yake. |
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana amewapongeza na kuwataka viongozi wote wanaochapa kazi na kuwataka waendelee kushirikiana kwa karibu na wananchi ili kuharakisha maendeleo.
Kinana ameyasema hayo Julai 27, 2022 mbele ya wana CCM na wananchi kwa ujumla wakati akikagua ujenzi wa Kituo Cha Afya cha Chapwa, kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe.
Makamu Mwenyekiti Kinana ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo hicho cha afya ambayo imeeleza kuwa ujenzi huo umetokana na ushirikiano wa wananchi na viongozi ambapo kwa pamoja kila mmoja alichangia kwa hali na mali kuhakikisha wanakikamilisha ili kujihakikishia upatikanaji wa huduma za afya karibu na makazi yao.
Kinana amesema ni lazima viongozi washirikiane na wananchi kwa kuwa hiyo ndiyo siri ya kufanikiwa katika jambo lolote, kwa kuwa wananchi wana mchango mkubwa katika kujiletea maendeleo yao binafsi na nchi kwa ujumla.
Kinana yupo mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 akitokea mkoani Rukwa.
Aidha, Kanali Kinana ambaye ameongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, kesho ataendelea na ziara hiyo mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment