Kampeni hii ilizinduliwa katika Soko la Karume na Afisa Mkuu wa Wateja binafsi na biashara wa NMB, Filbert Mponzi akishirikiana na Mkuu wa idara ya Bima wa NMB, Martin Massawe ikilenga kuongeza uelewa wa huduma za bima nchi kote sambamba na kupata Wateja wapya wa huduma hiyo.
Afisa Mkuu kitengo cha Wateja binafsi wa NMB, Filbert Mponzi alisema licha ya elimu juu ya bima kuongezeka, bado kuna watanzania wengi hawatumii huduma hizi. Takwimu zinaonesha ni asilimia 15 tu ya watanzania wanaotumia huduma mbalimbali za Bima.
Benki ya NMB inazo huduma tofauti za Bima inazoshirikiana na kampuni tofauti za Bima ambazo zinapatikana kwenye matawi 226 ya NMB nchini kote, mtandaoni kupitia Mkononi plus Kwa piga *150*68# au popote pale ulipo mpaka mahali ambako kampuni za Bima hazijafika.
Bima zinatolewa na Benki ya NMB ni Bima ya ujenzi, Afya, kilimo, Chombo cha moto, maisha, Mali n.k
Benki ya NMB imeshirikiana na kampuni zinazoaminika nchini ambazo ni Sanlam Life, Shirima la Bima la Taifa(NIC), Jubilee insurance, Jubilee life, Metropolitan life, Britain Insurance na shirima la Bima Zanzibar(ZIC) hivyo inauhakika ya kukidhi mahitaji yote ya wateja.
No comments:
Post a Comment