WANANCHI TUNDUMA NA TANGA WAPONGEZA HESLB KUSOGEZEWA HUDUMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 8 March 2022

WANANCHI TUNDUMA NA TANGA WAPONGEZA HESLB KUSOGEZEWA HUDUMA

Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wakisubiri huduma katika Banda la HESLB leo Jumanne Machi 8, 2022 wakati wa siku ya pili ya kampeni ya SIFURISHA inayolenga kuhamasisha urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu zinazoendelea katika  Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Tanga.

WAKAZI wa mji wa Tunduma ambao ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu wamepongeza uamuzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoa huduma za papo kwa papo kwa siku sita (06) katika viwanja vya Shule ya Msingi Tunduma kupitia kampeni ya SIFURISHA.

Kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wanufaika wa mikopo ya HESLB kujitokeza, kupata taarifa za madeni yao kwa njia ya mtandao au katika vituo vya mbalimbali na kulipa madeni yao hadi kufikia sifuri.

 

“Kwa kuja kwenu mmemaliza changamoto, nawapongeza sana kwani nilihitaji sana hii huduma na ninashauri muwafikie wengine kwa njia hii katika maeneo mengine,” amesema leo (Jumatatu, Machi 7, 2022) Mashaka Mwasumbi, Afisa Elimu Kata ya Chiwezi mjini Tunduma ambaye alinufaika na mkopo akiwa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ambako alihitimu mwaka 2013.

 

Kwa upande wake, Frida Muhindi ambaye ni Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji Tunduma amesema utoaji huduma kwa mtindo wa papo kwa papo unaofanywa na HESLB unawapunguzia gharama na usumbufu wanufaika ambao kutokana na majukumu ya kazi wanashindwa kufika katika ofisi za HESLB.

 

“Nilikua na changamoto katika deni katika mshahara wangu, nikawa nimepanga kwenda kwenye ofisi ya HESLB Mbeya lakini majukumu ya kazi yalinibana … kwa kufika hapa kumenisaidia san ana ninashukuru na kupongeza,” amsema Frida ambaye ailihitimu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo mwaka 2009.

 

Akizungumzia maoni ya wananchi, Meneja wa HESLB Kanda ya Mbeya, Anthony Ooko amesema lengo la kampeni ya #Sifurisha, pamoja na mambo mengine, ni kuwafikia na kuwahamasiha wanufaika wa mikopo popote walipo kujitokeza na kumaliza madeni yao.

 

“Tulianza kampeni hii mwaka jana ….wiki iliyopita tulikua Songea na Kahama na wiki hii tupo hapa Tunduma na wenzetu wapo Tanga na Morogoro hadi Machi 11 ambapo wanufaika wetu wanapata elimu na kuendelea kusifurisha,” miezi michache iliyopita inaendesha kampeni hiyo,” amesema Ooko na kuongeza:

 

“Katika kampeni hii, tunawakumbusha wanufaika kuwa wanaweza kupata taarifa za madeni yao kupitia mtandao kwa kutembelea tovuti yetu (www.heslb.go.tz), kubofya eneo la mnufaika au ‘Loan Beneficiary’ na kufuata maelekezo ili kupata deni lake na utaratibu wa kulipa … sio lazima kufika katika ofisi zetu,” amesema Ooko.

 

Kwa upande wake Meneja wa HESLB Kanda ya Arusha inayojumuisha Mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro, Patrick Shoo Kampeni ya SIFURISHA ina malengo ya kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa madeni ya mikopo ya elimu ya juu na kwa kutambua umuhimu huo HESLB imeamua kusogeza huduma hizo karibu zaidi kwa wateja wake.

 

Kampeni hii ni endelevu na tumeanzisha kampeni mahsusi kwa ajili ya kusogeza huduma zetu karibu zaidi na wateja wetu na hii inatusaidia kupokea  maoni, ushauri na hoja mbalimbali kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma zetu” amesema Shoo.

 

Kwa upande wake, Pricilla Kikoito, Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, ameipongeza HESLB kwa kusogeza huduma zake karibu zaidi na wananchi na kuiomba HESLB kuhakikisha kampeni ya SIFURISHA inakuwa endelevu ili kuwafikia wanufaika wengi zaidi wa elimu ya juu.

 

“TAMISEMI ina idadi kubwa ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu, tumekuwa tukitamani sana kufikiwa na huduma za HESLB katika maeneo yetu ya kazi, tumefurahishwa na huduma zinazotolewa na ikiwemo kupatiwa taarifa za madeni yetu ya mikopo na ufafanuzi wa hoja mbalimbali” amesema Pricilla.

 

Kampeni ya awamu ya Tatu ya SIFURISHA iliyoanza tarehe 28 Februari- 11 Machi mwaka huu inafanyika katika mikoa ya Morogoro, Tanga na Mbeya (Tunduma).  

 

Kampeni hiyo iliyoanza mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka jana tayari imefanyika katika Mikoa 6 nchini ambayo ni Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Geita, Zanzibar (Pemba) na Shinyanga (Kahama).

No comments:

Post a Comment