Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akitoa mpango mkakati wa kuinua elimu katika kikao hicho. |
Wakuu wa Wilaya za Singida wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Jerry Muro (Ikungi) Mhandisi Paskas Muragili (Singida Mjini) Sophia Kizigo (Mkalama) na Suleiman Mwenda (Iramba). |
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akizungumzia umuhimu wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwenye kikao hicho. |
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah akichangia jambo kwenye kikao hicho. |
Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya wakiwa kwenye
kikao hicho. Kutoka kushoto ni Hussein Simba (Itigi) James Mkwega (Mkalama)
Eliya Digha (Singida DC) na Jumanne Mlagaza.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KATIKA mwaka wa fedha 2022/23 Mkoa wa Singida umekadiria kutumia Sh. 261,012,288,000 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo ambapo Sh. 189,766,303,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida (Mishahara na Matumizi Mengineyo) Sh. 71,245,985,000 ni kwa miradi ya maendeleo.
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Singida, Beatrice Mwinuka wakati akitoa taarifa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa (RCC) kilichoketi leo mjini hapa.
Alisema kwa matumizi ya kawaida, Sh. 164,619,385,000 ni mishahara na Sh. 25,146,918,000 ni matumizi mengineyo.
Mwinuka alisema miradi ya maendeleo, Sh. 29,454,898,000 zinatokana na fedha za ndani na Sh. 41,791,087,000 ni fedha za nje.
Alisema kwa Sekretarieti ya Mkoa, Sh. 5,020,614,000 ni matumizi ya kawaida na kuwa Sh. 2,789,904,000 ni mishahara na Sh. 2,230,710,000 ni matumizi Mengineyo.
Alisema katika mwaka 2022/23, Mkoa umekadiria kukusanya jumla ya Sh. 18,274,735,000 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya ndani (Own Sources) ikiwemo Mapato halisi (Own Source Proper) Sh. 14,181,147,000 na Mapato lindwa Sh. 4,093,588,000.
Alisema kati ya fedha zitakazokusanywa kutoka mapato halisi, kiasi cha Sh. 5,672,458,800 zitatumika katika shughuli za Maendeleo na Sh. 12,602,276,200 zitatumika kugharamia Matumizi ya Kawaida.
Alisema Mkoa wa Singida unaomba
kuidhinishiwa jumla ya Sh., 261,012,288,000. Kati ya hizo Sh. 18,274,735,000
ni makusanyo ya ndani, Sh. 164,619,385,000 ni kwa ajili ya Mishahara,Sh.i
25,146,918,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo Sh. 71,245,985,000 kwa ajili ya Miradi
ya Maendeleo .
Aliongeza kuwa katika bajeti inayoandaliwa, fungu huwekewa ukomo wa bajeti,
ikiwa ni fedha za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Pamoja na ukomo kutolewa bado kuna uhitaji mkubwa, mkoa utawasilisha maombi
maalum yenye Jumla ya Sh.18,947,827,950.00 kwa ajili ya kuboresha ufanisi na kuongeza tija na maendeleo katika Mkoa
wa Singida.
Akizungumzia kuhusu suala la Anwani za Makazi na Postikodi Mwinuka alisema Halmashauri zimetoa mafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani wote, Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata na Watendaji wa vijiji wote.
Alisema Halmashauri zimefanikiwa kutambua taarifa za majina ya barabara, mitaa/vitongoji. Halmashuri ya Wilaya ya Mkalama, Manispaa, Manyoni na Ikungi. zimeshawasilisha makadirio ya Anwani ya makazi kwa Mratibu wa Mkoa na tayari zimeshatoa matangazo ya ajira ya muda na kufanya usaili.
Akizungumzia mpango wa matengenezo ya barabara kwa mwaka 2022/ 2023 kwa kila halmashauri kwa niaba ya Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Singida Meneja wa TARURA Manispaa ya Singida, Lambert Bayona alisema fedha zilizotengwa kutoka katika mfuko wa barabara kwa Manispaa ya Singida ni 1,248,630,00, maendeleo ya jimbo 500,000,000 na nyongeza bajeti na tozo ya mafuta ni Sh.500,000,000.
Alisema kwa Singida DC kutoka mfuko wa barabara ni Sh.668,030,000, maendeleo ya jimbo Sh.500,000,000 na nyongeza bajeti tozo ya mafuta, 1,000,000,000.
Kwa Ikungi fedha zilizotolewa kupitia mfuko wa barabara ni 881,040,000, maendeleo ya jimbo, Sh.1,000,000,000 na nyongeza ya bajeti tozo ya mafuta ni Sh. 2,000,000,000.
Alisema kwa wilaya ya Manyoni fedha kutoka mfuko wa barabara ni Sh. 706, 570,000, maendeleo ya jimbo Sh.500,000,000 na nyongeza ya bajeti tozo ya mafuta 1,000,000,000.
Iramba fedha za mfuko wa barabara ni Sh.824,920,000, maendeleo ya jimbo 500,000,000 na nyongeza ya bajeti tozo ya mafuta ni Sh.3,000,000,000 na Mkalama fedha za mfuko wa barabara ni Sh.658,840,000, maendeleo ya jimbo Sh. 500,000,000 na nyongeza ya bajeti na tozo ya mafuta ni Sh.1,000,000,000.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango na
bajeti ya mwaka 2021/2022 Meneja wa Wakala wa Maji
na Usafi wa Manzingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Singida Mhandisi Lucas Said
alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 mpaka kufikia februari 2022 kazi ambazo zimetekelezwa ni utafutaji wa vyanzo vipya vya maji na kupima
ubora wa maji ya vyanzo hivyo.
Alisema katika kipindi hicho jumla visima virefu 26 vimechibwa kwa gharama
ya Sh. 647,978,672 Ikungi kimoja kwa gharama
ya Sh.36,639,, Iramba 18 kwa gharama ya Sh.350,145,400, Manyoni viwili kwa
gharama ya 89,145,400, Mkalama 4 kwa gharama ya Sh. 136,833,272 na Singida DC kimoja
kwa gharama ya Sh.36,639,000 huku jumla yake ikiwa ni Sh.649,256,672.
Saidi alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 jumla Sh. 13,676,856,941. zilitengwa kw ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji na mpaka kufikia 28 februali. 2022, jumla Sh. 6,168,609,857 zimeshapokelewa sawa na 45% ya fedha zote.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akizungumzia mpango mkakati waliouwekwa wa kukuza taaluma mashuleni hasa shule za msingi alisema wamepanga kuboresha Mahudhurio ya Walimu na Wanafunzi ,Mazingira Rafiki kwa walimu na wanafunzi kuwa shuleni wakati wote wa masomo kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 8.30 mchana ,kukamilisha Miundombinu ,kutoa chakula ,kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi na kutoa huduma za bweni.
Mwaluko alisema mkakati mwingine walioupanga ni kuanza kutoa elimu kwa njia ya TEHAMA jambo litakalo saidia kuwafundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja hasa kwenye zile shule ambazo zinawafunzi zaidi ya 400 lakini wanafundishwa na mwalimu mmoja kutokana na Yule husika kutokuwa na walimu.
Alitaja malengo mkakati mengine kuwa ni kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo yote, masomo yote kufundishwa hata kama hakuna mwalimu katika shule, kuajiri walimu wa kudumu na kujitolea, kuimarisha uwezo wa walimu kitaaluma, kukuza matumizi ya TEHAMA,kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ,kusawazisha mtawanyo wa Walimu na Kutoa masomo katika Muda wa ziada.
Mwaluko aliutaja mpango mkakati wa tatu kuwa ni kuimarisha Uwajibikaji na Ushiriki,kuboresha uwajibikaji wa wasimamizi, jamii na wanafunzi,kuimarisha uwezo wa wasimamizi wa elimu ngazi zote, kusimamia nidhamu, wajibu na haki za walimu, kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa wanafunzi na kutoa elimu kwa jamii.
No comments:
Post a Comment