WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI SEKTA YA MISITU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 15 November 2021

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA KONGAMANO LA UWEKEZAJI SEKTA YA MISITU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizinduwa kongamano kubwa la uwekezaji katika sekta ya misitu Mkoani Iringa.

MKOA wa Iringa wenye kumiliki asilimia 40 ya misitu ya kupandwa nchini Tanzania na ni moja ya sehemu zenye aridhi bora sana kwa ajili ya kilimo cha miti duniani. Ili kutumia fursa hii mkoa wa Iringa umeandaa kongamano kubwa la uwekezaji katika sekta ya misitu.

Akifungua kongamano hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa pongezi kubwa kwa mkoa na pia kueleza msimamo wa Serikali ya awamu ya sita katika kuchochea uwekezaji nchini. Pia Waziri Mkuu aliagiza makampuni yenye kuchakata mazao ya misitu kuhakikisha yanatengeneza bidhaa bora na kutosafirisha bidhaa ghafi.

Waziri Mkuu aliuelezea mkoa wa Iringa kama eneo bora la uwekezaji likiwa na muunganiko mzuri wa barabara na muda mfupi ujao kwa ndege baada ya kukamilika kwa uwanja wa ndege wa Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendega alisema mkoa wake uko tayari kusaidia wafanya biashara kufanya biashara kwa urahisi kwa kuweka mazingira wezeshi.

Kabla ya kufungua kongamano hilo alizindua chapa ya Iringa woodland ikiwa ni lengo la mkoa wa Iringa kuchagiza ukuaji wa utengenezaji wa bidhaa za mbao, kuutangaza mkoa na pia utalii. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Gofin Ventures Imani Kajula ambao ni waandaaji wa kongamano hilo na mkakati wa kujenga chapa ya Iringa woodland alisema " hii ni fursa pana kwa mkoa wa Iringa kufaidika na sekta ya utalii, misitu na pia kuutangaza mkoa wa Iringa ndani na nje ya Tanzania" pia kutoa ajira kwa vijana ambao watatumia chapa ya Iringa woodland kutengeneza bidhaa mbali mbali.


Matukio picha mbalimbali katika kongamano la uwekezaji sekta ya misitu linalofanyika Mkoani Iringa.


Matukio picha mbalimbali katika kongamano la uwekezaji sekta ya misitu linalofanyika Mkoani Iringa.


No comments:

Post a Comment