*Ni baada ya kutanua kiwango cha matumizi hayo kwa 104%
*Yawa ya kwanza kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kupitia POS
BENKI ya NMB imekuwa ya kwanza nchini Tanzania kutunukiwa tuzo ya benki kinara katika ukuzaji wa ongezeko la watumiaji wa kadi kwa zaidi ya asilimia 100, iliyotolewa na MasterCard International, baada ya kutanua kiwango cha matumizi kwa asilimia 104 kwa mwaka 2021.
Meneja Mkazi wa MasterCard International – Kanda ya Afrika Mashariki, Shehryar Ali, amesema Benki ya NMB yenye wateja zaidi ya milioni 4 nchini, imetunukiwa tuzo hiyo kwa sababu mbili, kuu ikiwa ni idadi kubwa ya wateja wanaotumia kadi kuliko benki yoyote Tanzania.
Shehryar amesema kuwa, mbali ya kuwa kinara wa uhamasishaji wa matumizi ya kadi, ambao Ni rahisi, nafuu na salama – kupitia kampeni za NMB MastaaBoda, NMB MastaBata na nyinginezo, pia benki hiyo imekuwa ya kwanza kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kupitia Vituo vya Mauzo (POS).
“Leo tuko hapa kufurahia tuzo itokanauo na rekodi kubwa ya ukuaji wa matumizi ya bidhaa za MasterCard bkwa wateja wa NMB. Tunasherehekea dira sahihi ya kimapinduzi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB (CEO), Ruth Zaipuna, Maofisa na Watendaji wengine wa benki hii.
“Zaidi ya hapo, mafanikio haya hayatokani tu ubunifu wa kihuduma uliofanywa na NMB, bali yanatokana na idadi kubwa ya wateja waliohamasika kutumia huduma hizo zinazohusisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu,” amebainisha Shehryar kabla ya kukabidhi tuzo hiyo.
Naye Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, alikiri kufurahia mafanikio hayo, sambamba na kupokea tuzo hiyo kwaniaba ya benki yake, ambayo anaamini imetokana na washirika wao hao kibiashara kutambua na kuthamini mchango wa taasisi yake katika kukuza matumizi ya kadi nchini.
“Tuzo hii ni uthibitisho juu ya ukubwa wa benki ya NMB unaojumuisha sio tu mtaji mkubwa, bali pia mtandao mpana wa matawi zaidi ya 226 na wateja zaidi ya milioni 4 kote nchini. TUNAWASHUKURU wateja wetu kwa mwitikio uliotufanya kutambuliwa na MasterCard kiasi cha kutunukiwa tuzo hii ambayo nibya kwanza kutwaliwa na benki yoyote nchini.
“NMB tuna wateja zaidi ya milioni 3 wanaotumia Kadi za MasterCard kwa huduma mbalimbali za kifedha, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kufikiwa na benki yoyote Tanzania. Pia sisi ndio vinara wa kutanua ongezeko la watumiaji wa kadi, tulikofikia asilimia 104 kwa mwaka huu unaoelekea mwisho,” amefafanua.
Mponzi ameahidi kwamba NMB itaendelea kuwa kinara wa ubunifu wa suluhishi zenye kuboresha matumizi ya kadi na kwamba wanafurahishwa na utambuzi wa mapinduzi chanya Kidijitali uliofanywa na MasterCard, huku wakiamini kuwa idadi ya watumiaji wa kadi itaongezeka kwa Kasi zaidi.
Aidha, Mponzi alifichua kuwa NMB inajisikia fahari kubwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na MasterCard, ambao teknolojia yao na ubobevu wao katika mifumo ya matumizi na malipo kwa njia ya kadi ni bora na yenye kutambuliwa ulimwenguni kote na kwamba imewasaidia kuwarahisishia utoaji huduma.
No comments:
Post a Comment