MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla ameungana na wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Pemba, wananchi na wateja wa benki hiyo, katika futari maalum iliyoandaliwa na NMB kwa wateja wao.
Alisema kuwa NMB kufutari pamoja na wateja wao ni jambo la kupongezwa na kuungwa mkono na mabenk mengine, kwani kuna wafanya wateja kuwa karibu na benk hiyo katika kufikisha changamoto zao.
“Funga ni nguzo katika nguzo za uislamu, kufutari pamoja ni jambo la muhimu hata Mtume ameligusia, hongereni NMB kwa kuwafutarisha wateja wenu,” alisema.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa futari hiyo, iliyofanyika Mjini Chake Chake, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Afisa Mdhamini wizara ya Fedha na Mipango Ibrahim Saleh Juma, aliwataka NMB kuzidisha ushirikiano na jamii kwa ujumla, ili kuwafanya wateja wengine kuweka amana zao katika benki hiyo.
Alisema mashirikiano yakipatikana kutawafanya wafanya biashara kuhamasika zaidi, kufungua akauni zao katika benk hiyo na kuweka amana zao, kwani ndizo zinazopelekea benk kuendelea kuwepo.
“NMB ni miongoni mwa benk kongwe katika kisiwa cha Pemba, tokea mwaka 1995 ilianzishwa imekuwa ikisaidia huduma mbali mbali za jamii, vizuri na sisi wananchi tukaendelea kuiyunga mkono katika kuweka amana zetu," alisema.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwasihi wananchi kuzidisha usafi wa mazingira katika maeneo yao wanayoishi, katika kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea, sambamba na kuweka vyakula vyao vizuri katika mazingira salama.
Akizungumzia suala la amani na utulivu, aliwataka wananchi kuendelea kushikamana na kuwa wamoja, kwani amani ndio kitu muhimu pekee duniani.
Alisema kuna nchi nyingi duniani hivi sasa zinaishi katika mazingira magumu baada ya kuipoteza amani hiyo, hivyo aliwapongeza viongozi wa nchi akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kusimamia amani hiyo.
Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salam na Zanzibar Badru Iddi, alisema kuwa NMB itaendelea na utaratibu wake wa kufutari pamoja na wateja wake Tanzania nzima kila mwezi wa Ramadhani unapofika, kwani kufutarisha ni jambo la muhimu sana katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Hata hivyo aliwahakikishia wateja na wananchi wa Kisiwa cha Pemba, wataendelea kutoa huduma bora kwa vile wanavyohitaji wananchi na wateja wao.
Mapema meneja wa NMB Tawi la Pemba Ahmed Nassor, alisema NMB Pemba wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora ili kuwaleta karibu wananchi na kujiunga katika benk hiyo pamoja na kuweka amana zao.
Akitoa neneo la shukurani kwa niaba ya wananchi wa Kisiwa cha Pemba, Naibu Mufti wa Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa Wadi, alisema NMB imefanya jambo kubwa kwa kuonyesha hisia zao moja kwa moja kwa wananchi kufuatia kufutari nao pamoja.
No comments:
Post a Comment