Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son wakionesha namna mteja wa halotel anavyoweza kunufaika na huduma hiyo mpya. |
KAMPUNI ya Halotel Tanzania imekuja na huduma mpya ya mawasiliano iitwayo ‘MPANGO MZIMA’ ambayo pamoja na faida zake nyingine inamuwezesha mtumiaji wa simu wa mtandao wa Halotel kupata unafuu katika huduma mbalimbali za simu.
Kuanzishwa kwa huduma ya Mpango Mzima ni muendelezo wa kampeni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Halotel katika kumrahisishia mteja wake kupata huduma bora za mawasiliano zikiwemo za kutumia Intaneti bila kikomo, kupiga simu matandao yote bila kikomo, kutuma ujumbe mfupi wa maneno(sms),
Akiziungumza kuhusu ‘Mpango Mzima’ Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son alisema ujio wa huduma hiyo mpya na ‘Kijanja’ imelenga kumwezesha mtumiaji wa mtandao huo kutumia intaneti yenye kasi na ukubwa wa (GB 5) bila kikomo.
Pamoja na Intaneti hiyo mtumiaji wa mtandao huo pia ataweza kupiga simu kwenda mitandao yote bure kwa kila dakika 5 za kwanza pamoja kuzawadiwa sms 5000 atakazozitumia katika kipindi cha mwezi mzima.
“Huu ni muendelezo wa mpango wa mapinduzi ya kimawasiliano wa Halotel kuwa karibu na kuwajali wateja wetu kwa huduma bora. Kuanzishwa kwa Mpango Mzima kutamwezesha mteja wetu wa Halotel kutumia intaneti ya kasi kubwa , kupiga simu bila kikomo kwa mitandao yote bure kila dakika 5 za mwanzo na hivyo kumuondolea hofu ya simu kukatika kabla hajamaliza maongezi” amesema Son.
Amesema ili mteja aweze kufaidika na huduma hiyo mpya anapaswa kujiunga kwa kupiga *148*66# na kuchagua Mpango Mzima ambapo ataweza kujiunga na kuwa tayari kwa kuanza kufurahia unafuu huo mahususi kwa ajili ya watumiaji wa mtandao wa Halotel.
Mkurugenzi huyo Bw. Nguyen Van Son amesema huduma ya Mpango Mzima ni mpya kuwahi kutolewa na mtandao mwingine wowote wa simu hapa nchini na kuwaambia watumiaji wa Halotel kuwa hiyo ni zawadi kwao hivyo wanapaswa kuifurahia na kuitumia wakati wote.
Aidha Mkurugenzi huyo Bw. Nguyen Van Son wa alisema Halotel pia imeweza kuunganisha Optic Fiber zenye urefu wa zaidi ya Kilomita 20,000 katika maeneo yenye miundombinu yake kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa data kwa maeneo mapya na hivyo kuiwezesha kuwa chaguo la kwanza kwa wateja pale linapokuja suala la huduma za Internet.
No comments:
Post a Comment