RAIS DK MAGUFULI HUYOOO AFRIKA YA KUSINI NA JK...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 24 May 2019

RAIS DK MAGUFULI HUYOOO AFRIKA YA KUSINI NA JK...!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wakiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwa ameongoza na na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula wakielekea kwenye ndege  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Myerere jijini Dar es Salaam tayari kuelekea Afrika ya Kusini asubuhi hii ambapo kesho watahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa mjini Pretoria. Picha na IKULU.

No comments:

Post a Comment