|
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akishuhudia tukio hilo. |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia). |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaotoa huduma ndani ya duka hilo jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam. |
|
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL, Mhandisi Omary Nundu akimsikiliza. |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akiingia kwenye duka hilo mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi. |
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba (wa pili kushoto) wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar Es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela. |
|
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam. |
|
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam. |
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo limezinduwa duka
jipya na kituo cha huduma Kariakoo eneo la Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar
es Salaam ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu alisema kwa Mwaka
2019, TTCL imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Huduma za Shirika hilo zinasambaa
zaidi kote nchini huku ikisimamia ubora na unafuu wa gharama ambazo zitakuwa nafuu
kwa wananchi.
"...Tunakusudia kuendelea kufanya mageuzi makubwa ndani
ya Shirika ili kuliwezesha kushindana kikamilifu katika Soko la Huduma za
Mawasiliano Nchini sambamba na kutimiza wajibu wa kimsingi wa kuwa mchangiaji
muhimu katika Pato la Taifa," alisema Mhandisi Omary Nundu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw.
Waziri Waziri Kindamba awali akizungumza alisema uzinduzi huo wa duka na kituo
cha Huduma kwa Wateja ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu,
2016-2019 ambao umeweka msisitizo mkubwa katika kuboresha eneo la Huduma kwa
Wateja.
"Uzinduzi wa leo unaonesha kwa vitendo jinsi gani TTCL
mpya ilivyojipanga vyema kuhakikisha huduma zake zinawafikia Wateja katika
mazingira mazuri, yanayovutia na kuwakilisha hadhi ya Shirika letu. Kukamilika
kwa Duka hili/ Kituo hiki cha Huduma kwa Wateja kuonaongeza idadi ya Maduka
mapya ya TTCL kufikia maduka 10 ambayo yamejengwa kwa viwango vya hali ya juu
na kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya utoaji bora wa Huduma kwa Wateja,"
Aidha aliongeza kuwa TTCL itaendelea kuboresha Maduka na
Vituo vyetu Nchi nzima, sambamba na Ofisi zake za Mikoani na Wilayani ili
ziweze kuwa mahali bora kabisa kwa Watumishi wa TTCL wanaotoa huduma na Wateja
wote watakaofika kupata huduma za aina mbalimbali.
No comments:
Post a Comment