Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Posta la nchini Burundi limewekabayanadhamirayake ya kushirikiana na Tanzania katika kukuzasekta ya Posta nchinihumo ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi zaidi katika usimamizi wa masuala ya Posta.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Posta wa Burundi, Bi. Lea Ngabire wakati alipozuru Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akiambatana na ujumbe wa Maafisa waandamizi wa Posta Burundi katika ziara ya mafunzo.
“Tumefikahapa TCRA na kujionea shughuli mbalimbali za mawasiliano na lengo letu ni kuona namna nchi zetu mbili zinavyoweza kushirikiana katika kukuza na kuendeleza sekta ya posta,” alibainisha Ngabire.
Ujumbe wa Maafisahaoumejumuisha Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Posta Burundi Nyayishimiye Olivier na Mkuu wa masuala ya Barua Misirakuba Deo.
Akipokea ujumbe huo mnamo Jumatano Tarehe 17 Novemba 2021 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt. Jabiri Bakari aliwakaribisha na kuwaeleza kuwa TCRA kama mdhibiti wa sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania inatambuaumuhimu wa ushirikiano wa mawasiliano hasa kikandana imekuwa mshirika muhimu wa mawasiliano katika ukanda wa AfrikaMashariki.
“Lengo letu ni kuhakikishasekta ya mawasiliano nchini Tanzania inasimamiwa kwa uthabiti na kwa upande wa posta TCRA imekuwa ikishirikiana na taasisimbalimbali za kikanda na kimataifa na kama mnavyofahamu pia MakaoMakuu ya Posta Afrikayapohapanchini” alibainisha na kuongeza Jabiri.
Pembezonimwa mazungumzo na ujumbe huo pia, Mkurugenzi Mkuu Jabiri aliwaeleza wajumbe hao kwamba Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikishasekta ya mawasiliano barani Afrika inaimarika na ndiyosababu imekuwa ikishirikiana na Shirika la Posta Afrika (PAPU) kuhakikishaujenzi wa Ofisi ya PAPU makaomakuu ambayo ujenzi wake unaendelea jijini Arusha unakamilika kwa wakati ambapomatarajio ni kukamilishaujenzi wa jingo la kisasajijini Arusha itakapowadia 2022.
Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta wa TCRA, Dkt. Emmanuel Manasseh ambae sekta ya Posta inasimamiwa na kurugenzi anayoingoza alibainisha kwamba hakuna namna uchumi wa kisasa utajengwa bila kuhusisha posta kwani sekta hiyo ni muhimu katika masuala ya usafirishaji na ufikishaji wa taarifa mbalimbali zinazowezesha kujenga uchumi wa kisasa (Uchumi wa kidijitali).
No comments:
Post a Comment