TPA WATAKIWA KUJIPANGA KUFANYA BIASHARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 14 October 2021

TPA WATAKIWA KUJIPANGA KUFANYA BIASHARA


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw, Adam Malima akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (kulia), walipokagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya bandari ya Tanga (katikati), ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw, Donald Ngaile.


Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Tanga Bw, Musa Mchola akiwaonesha mpaka wa uwanja huo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa (kulia),  na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw, Adam Malima (kushoto), walipoukagua.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Tanga mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Tanga, wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw, Adam Malima na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw, Donald Ngaile.


Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw, Donald Ngaile akiwaongoza Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kukagua ujenzi wa miundombinu ya bandari hiyo.

Msimamizi wa Ujenzi wa Bandari ya Tanga Eng. Abdala Othman Mwinyi akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa alipokagu maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya bandari ya Tanga (kushoto), kwa Waziri ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw, Adam Malima na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Bw, Donald Ngaile.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw, Adam Malima walipokagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Bandari ya Tanga.


WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Bandari nchini kujipanga kufanya biashara ili kukidhi malengo ya Serikali ya kutumia lango la bandari kukuza uchumi wa nchi na wakazi wake.

Amesema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga na kukarabati miundombinu ya bandari hivyo ni wakati sasa kwa watendaji na watumishi wa bandari kuleta biashara kubwa nchini itakayoleta faida na kuhuisha uchumi wa sekta nyingine.

“Ni wakati wa idara ya masoko ya bandari na watumishi wake kufanya kazi kimkakati wakilenga kufanya biashara na kuzalisha faida”, amesema Prof. Mbarawa.

Amezungumzia umuhimu wa watendaji wa bandari kuweka wahitimu wa fani za uhandisi katika miradi ya ujenzi inayoendelea ili kuwajengea watanznia uwezo.

Zaidi ya shilingi bilioni 440 zitatumika katika ukarabati mkubwa wa bandari ya Tanga na kukamilika huko kutawezesha meli nyingi na kubwa kutumia bandari hiyo na kufufua uchumi wa mkoa huo.

Amezungumzia umuhimu wa uadilifu, ubunifu na uzalendo kwa watumishi wa bandari ili waweze kushindana na bandari nyingine na kupata tija.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw, Adam Malima amemhakikishia Waziri wa Ujenzi  na Uchukuzi kuwa mkoa huo utahakikisha unaweka mazingira salama na rafiki kwa wakandarasi wanaojenga miundombinu mkoani humo ili kufikia malengo ya kimkakati ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Prof. Mbarawa alikuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Tanga kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, vivuko, uwanja wa ndege na bandari. 

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI


No comments:

Post a Comment