Wafanyakazi wa NMB 'Bank House'. |
WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB matawi la Clock Tower, Kenyatta, Bank House na Madaraka wameungana na wananchi wengine kuadhimisha Wiki ya Maziwa hapa nchini inayohamasisha matumizi zaidi ya unywaji wa maziwa.
Katika tukio hilo, wafanyakazi walipata nafasi ya kunywa maziwa na mazao mengine yatokanayo na maziwa yanayozalishwa na kampuni ya Kilimanjaro Fresh na Tanga Fresh huku wakizingatia kanuni zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona.
Meneja Uhusiano Mwandamizi wa NMB Kanda ya Kaskazini anayeshughulikia Kilimo- Oscar Rwechungura alisema katika kuadhimisha Wiki ya Maziwa kwa kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya maziwa wanawezesha sekta hiyo katika mnyororo wa thamani.
Wafanyakazi wa NMB Clock Tower. |
Wafanyakazi wa NMB Kenyatta. |
Wafanyakazi wa NMB Madaraka. |
Alisema lengo la NMB ni kupanua wigo kwa wafugaji wadogo ili waweze kupata huduma za kifedha kwa njia rahisi ili kuongeza idadi ya ng’ombe, vyakula vya mifugo na huduma za matibabu ya mifugo ili kuongeza tija ya ufugaji wao.
“Lengo letu ni kuwawezesha wazalishaji wa maziwa kuongeza tija, badala ya mfugaji kutegemea kupata maziwa lita mbili kwa siku jambo ambalo halimfanyi aone faida ya kazi anayoifanya tunatamani apate lita 20 na zaidi kwa siku hivyo ili mfugaji apate faida lazima aongeze matumizi kwa kupata uwezeshwaji kutoka kwetu,”
NMB haishii kuwawezesha wafugaji wadogo na kati kupata mitaji pekee bali inawaunganisha na masoko ili kuwezesha mnyororo wa thamani katika sekta nzima ya maziwa kuanzia kwa mfugaji hadi anayepeleka maziwa sokoni.
No comments:
Post a Comment