OLE SABAYA AKUTWA NA HATIA, AMTAJA MCHUMBA WAKE KWA UTETEZI...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 15 October 2021

OLE SABAYA AKUTWA NA HATIA, AMTAJA MCHUMBA WAKE KWA UTETEZI...!

Mshtakiwa, Lengai Ole Sabaya (katikati)

HAKIMU Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema mshtakiwa Lengai Ole Sabaya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai amekutwa na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili pamoja na wenzake. Hakimu amesema hayo Oktoba 15, 2021 wakati akiendelea kuchambua hoja wakati akisoma hukumu ya Sabaya na washitakiwa wenzake watatu.

Sabaya baada ya kukutwa na hatia anaiomba mahakama imuonee huruma kwani sio yeye bali alikuwa anatekeleza maagizo ya Mamlaka yake ya Uteuzi, pamoja na hayo mshtakiwa huyo anabainisha ana mchumba walikuwa wafunge ndoa na mahari ameshatoa.

Awali Hakimu Amworo amesema hakuna shaka washitakiwa watatu walifika dukani kwa Mohamed Saad siku ya tukio. Ameongeza kuwa amethibitisha mshitakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya na mshitakiwa wa pili Sylivester Nyegu walikuwa wanafahamiana.

Ameeleza kuwa imethibitika mshitakiwa wa kwanza alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

Hata hivyo, amesema hakuna silaha iliyotumika katika tukio hilo, hivyo hakuna shambulizi la kutumia silaha. Hakimu amesema kati ya mashahidi 11 waliotoa ushahidi wao dhidi ya Sabaya, ni mashaidi wawili tu ndio ambao ushahidi wao haukuwa na mashiko. 

Sabaya amekutwa na hatia kabla ya kupewa nafasi na watuhumiwa wenzake wajitetee ili Wapungiziwe adhabu.

No comments:

Post a Comment