SHULE ya Msingi Wilolesi Mkoani Iringa Imepokea msaada wa masinki 15 ya vyoo kutoka Duka la vifaa vya Ujenzi la Dar Ceramica Centre lililopo Manispaa ya Iringa msaada ulilenga kupunguza tatizo la uchakavu wa vyoo katika shule hiyo na kuwaondosha wanafunzi katika hatari ya kukabiliwa na magonjwa mbalimbali yatokanayo na ukosefu wa vyoo bora.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la Dar Ceranica Centre lililopo katika manispaa ya Iringa,meneja mauzo wa kanda ya kusini John Gondwe alisema kuwa wamefungua tuka hilo kwa lengo la kuwafikishia huduma ya vifaa bora vya ujenzi wakazi wa mikoa ya nyanda za juu kusini.
Alisema kuwa wanauzoefu wa kuuza vifaa hivyo bora zaidi nchini kwa zaidi ya miaka 25 ambapo wamefanikiwa kufungua jumla ya maduka 11 ambayo yanauza vifaa vya ujenzi hapa nchini Tanzania.
Gondwe alisema kuwa wameamua kutoa msaada wa masinki 15 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule ya msingi Wilolesi baada ya kugundua kuwa shule hiyo ina vyoo chakavu ambavyo sio rafiki kwa matumizi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Alisema kuwa duka hilo limekufunguliwa mkoani Iringa kwa lengo la kuwarahisishia wananchi kupata vifaa bora ya ujenzi ambavyo kwa asilimia kubwa vinatoka nje ya nchi.
Gondwe alisema kuwa wanavifaa bora na Imara vya ujenzi kama vile tiles kutoka Hispania,bomba,miksa,beseni,bathtubs na Jacuzzi kutoka nchini Ureno,mashine za kuchemshia maji ya moto vyooni au bafuni kutoka katika nchi ya Itali na vifaa vyote vinavyonunuliwa katika duka hilo vinakuwa na warranty ya uhakika.
Alisema kuwa duka hilo limekuja na neema kwa mafundi ujenzi wa mkoa wa iringa na nje ya mkoa wa Iringa kwa kuwa uongozi wa duka hilo umeamua kuwapatia elimu ya kuongea ujuzi wa ufundi wao.
Aidha Gondwe alisema kuwa fundi Lazaro Mwinuka ameibuka mshindi wa shindano la Serereka na Dar Ceramica wa mkoani Iringa kwa kupata zawadi ya vifaa vyote vya ujenzi ambavyo vitamsaidia kuongeza ufanisi wa kazi zake.
Gondwe alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa kwenda kununua vifaa bora na Imara kutoka katika duka la Dar Ceramica Center ambalo lipo katika jengo la Hanspoppe mkabala na hotel ya M.R.
Kwa upande wake mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa wamebahatika kupata duka ambalo linauza vifaa bora na imara vya ujenzi mkoani humo.
Alisema kuwa amefanikiwa kuviona vifaa hivyo ambavyo vinauzwa kwenye duka hilo kuwa ni vifaa vyenye ubora na imara kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali kwa gharama nafuu kabisa.
Msambatavangu alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kunaongeza ajira kwa wananchi wa jimbo la Iringa Mjini na maeneo ya jirani kwa kuwa mafundi wote watakuwa wanapata kazi nyingi kwa kuwa wanakuwa wanatumia vifaa bora na imara kutoka katika duka la Dar Ceramica Center lililopo manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa faida nyingine ambayo inapatika kwa uwepo wa duka hilo ni kuinua kiwango cha uchumi kwa kushirikiana na jamii ambayo ndio watakuwa wateja na watumizi wa vifaa hivyo.
Msambavangu alisema kuwa amejitolea kuwa balozi wa duka hilo na kuwaomba wananchi wengine kujitolea kulitangaza duka hilo lenye vifaa bora na imara vya ujenzi kwa wananchi wote wa mkoa wa Iringa na nje ya Iringa.
Naye balozi wa maduka ya Dar Ceramic Center,Irene Paul aliwataka wakazi wa mkoa wa Iringa kununua vifaa bora na imara vya ujenzi katika duka hilo ambalo limefunguliwa katika manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa
kufunguliwa kwa duka hilo kunaleta fursa kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kwa
kuweza kununua vifaa vya ujenzi vilivyo bora na imara kwa gharama nafuu na
vyenye warranty ya uhakika.
No comments:
Post a Comment