RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWAAPISHA VIONGOZI WAWILI IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 28 September 2021

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWAAPISHA VIONGOZI WAWILI IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

 

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Mathew Modest Kilama akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini Togolani Edriss Mavura wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 27 Septemba, 2021. PICHA NA IKULU.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Togolani Edriss Mavura kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 27 Septemba, 2021.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mathew Modest Kilama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 27 Septemba, 2021.


No comments:

Post a Comment