SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA BORA KUKUZA VIWANDA NA BIASHARA - WAZIRI PROF. MKUMBO - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 13 July 2021

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA BORA KUKUZA VIWANDA NA BIASHARA - WAZIRI PROF. MKUMBO

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akizungumza katika Kikao cha pamoja kati ya Serikali na  Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini kilichofanyika  leo 12/07/2021 Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.


Sehemu ya wajumbe wa Kikao cha pamoja kati ya Serikali na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini kilichofanyika  leo 12/07/2021 Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.


Kikao cha pamoja kati ya Serikali na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini kilichofanyika  leo 12/07/2021 Benki Kuu, jijini Dar es Salaam kikiendelea.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amesema Serikali imepanga kuweka mazingira bora ili kuendeleza na kukuza Sekta ya Viwanda na Biashara ili iwe na mchango mkubwa katika  pato la Taifa.

Waziri Mkumbo ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mpango wa utekelezaji wa bajeti pamoja na maeneo ya ushirikiano yaliyopo katika Sekta ya Viwanda na Biashara  katika  Kikao cha pamoja kati ya Serikali na  Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini kilichofanyika  leo 12/07/2021 Benki Kuu, jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha maeneo ya ushirikiano katika kikao hicho kililcholenga kuwapitisha wajumbe hao katika Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22, Mipango ya utekelezaji  pamoja na maeneo ya ushirikiano, Prof. Mkumbo amesema Tanzania itaendeleza makubaliano ya kibiashara baina ya Nchi na Nchi, Kikanda na Kimataifa kupitia majukwaa mbalimbali ya kibiashara ili kukuza biashara ndani na nje ya nchi.

Akitaja vipaumbele 10 vilivyoainishwa katika Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2021/22 pamoja na programu 15 za utekelezaji, Prof. Mkumbo amesema, Wizara imeanzisha mpango maalum wa kuhamasisha bidhaa zinazozalishwa nchini kutumika nchini na kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo kwa ajili ya mauzo ya nje ya nchi.

Aidha, Prof Mkumbo amesema  kuwa Serikali inachukua hatua mbalimbali katika kuboresha mazingira  na kurahisisha ufafanyaji biashara nchini ikiwemo kurekebisha sheria mbalimbali pamoja na kubadili mtazamo na utendaji kazi wa watumishi katika sekta hiyo ili  kuwawezesha na kutoa huduma bora kwa wafanyabiashara.

Waziri Mkumbo pia amewasihi wajumbe wa kikao hicho kuendelea kisaidia sekta binafsi ambayo bado ni changa ili iweze kufanya biashara kwa ufanisi kwa kuzingatia sheria na weledi ili kukuza uchumi wa nchi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Maliasili na Utalii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Nchini.

Aidha, Mawaziri walioshiriki kikao hico walipata fursa ya kuwasilisha mipango ya utekelezaji ya bajeti, vipaumbele na maeneo ya ushirikiano katika Sekta zao na wajumbe wote walipata fursa ya kujadili kutoa maoni na mapendekezo katika sekta husika.

No comments:

Post a Comment