SHULE YA ECKERNFORDE TANGA YATEKELEZA MAONO YA RAIS SAMIA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 31 August 2026

SHULE YA ECKERNFORDE TANGA YATEKELEZA MAONO YA RAIS SAMIA

 

Kaimu Mwenyekiti wa mtandao wa wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali nchini Tanzania (TAMONGSCO), Mwalimu  Methew Levi Alex ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza kwenye mahafali ya wanafunzi wa darasa la awali, darasa la saba na kidato cha nne katika Shule za Eckernforde yaliyofanyika Agosti 29, 2026 Jijini Tanga.

Na Dotto Mwaibale, Tanga

SHULE ya Mchepuo wa Kiingereza ya Eckernforde ya Jijini Tanga emeelezwa ni miongoni mwa shule inayotekeleza maono ya Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya kuona wanafunzi wanafundishwa na kuelewa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mwenyekiti wa mtandao wa wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali nchini Tanzania (TAMONGSCO), Mwalimu  Methew Levi Alex ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya wanafunzi wa darasa la awali, darasa la saba na kidato cha nne wa Shule za Eckernforde yaliyofanyika Agosti 29, 2026 Jijini Tanga.

“Nimeona maonesho mbalimbali ya kitaaluma ambayo wahitimu wameyafanya  katika mahafali haya niwapongezeni sana na hali hii inaonesha namna mlivyopiga hatua hakika mnakwenda na maono ya Rais wetu Dk. Samia ambaye anataka kuona wanafunzi wanafundishwa na kuelewa,” alisema Alex.

Alex aliwaeleza wahitimu hao kuwa kumaliza kidato cha nne ndiyo maandalizi ya kuingia kidato cha tano na sita hivyo wajiandae vizuri.

Alisema watakapo kuwa nyumbani watumie muda huo kwa kujisomea na kujihadhari na matumizi ya mitandaa ya kijamii kama tiktok kuangalia mambo ya hovyo.

“Chukueni tahadhari ya matumizi ya mitandao ya kijamii yatawapotezea muda wenu wa kujisomea hivyo mjidhatiti kwenye masomo yenu kwani elimu ndiyo msingi wa maisha yenu ya baadaye,” alisema Alex.

Akiwazungumzia walimu alisema wanapaswa kuzingatia mambo matatu ambayo ni uwajibikaji, maadili pamoja na kufuata sheria na miongozo yote iliyowekwa.

Katika hatua nyingine aliwataka wazazi na walezi kujenga tabia ya kuwafuatilia watoto wao ili kubaini watoro shuleni badala ya kuwaachia walimu kwa madai ni jukumu lao baada ya kuwalipia ada.

Alex alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wazazi kujenga tabia ya kulipa ada kidogo kidogo hata kwa kutoa shilingi 1000, 5000 na kuendelea jambo litakalowasaidia kuwaondolea usumbufu wa kulipa fedha nyingi pale wanaposubiri shule zifunguliwe.

Mkuu wa Sekondari ya Eckernforde, Salum Massesa akizungumzia historia ya shule hiyo alisema Shule ya Msingi ilianzishwa na Mkurugenzi mwanzilishi Hayati Remency Shikusiry Tarimo mnamo mwaka 1999 na sasa inaongozwa na mkurugenzi mwendeshaji ndugu Omary Mbogo.

Alisema kwa sasa ni miaka 27 tangu ilipoanzishwa na pia alianzisha shule ya Sekondari mwaka 2006 ambapo sasa ni miaka 20 tangu ianzishwe.

Massesa alisema shule hizo mbili, kwa sasa zina jumla ya walimu 43, wanaume 36 na wanawake 17 ambao ni walimu waliobobea na wenye sifa za kutosha.

“ Na kauli mbiu yetu ni “Elimu bora” kwa mtoto wa Kitanzania na si “Bora Elimu,” aalisema.

Massesa alisema kuwa Walimu wanajituma na hakika wanaienzi vilivyo kazi yao kwa weledi mkubwa na kueleza kuwa wana  wafanyakazi wasio walimu 38, wanaume 17 na wanawake 21. 

Aidha, Massesa alisema Shule ya Msingi kwa sasa ina wanafunzi 790, wasichana 375 na wavulana 415. Wana wanafunzi kuanzia Chekechea (Nursery) hadi darasa la saba.

Alisema kwa upande wa Shule ya Sekondari kwa sasa ina wanafunzi 164 wasichana 91 na wavulana 73.

Alisema wana wanafunzi wa Kidato cha kwanza hadi kidato cha nne, Wapo wanaolala shuleni (boarding) na wengine ni wakutwa (day).

Mwalimu Massesa alisema wanapokea wanafunzi kutoka Mikoa yote, Mataifa yote na Dini mbalimbali.

Aliongeza kuwa Shule ya Sekondari imefanikiwa pia kuanzisha kituo cha Wanafunzi wa kujitegemea chenye watahiniwa 50 watakaofanya mtihani mwaka huu.

MAFANIKIO.

Massesa aliongeza kuwa Shule yao imepata mafanikio makubwa katika mitihani ya darasa la saba tukianzia na Mock – Wilaya hadi Mkoa kwa ufaulu wa asilimia mia.

"Shule yetu haijawahi kufelisha wanafunzi. Mwaka jana matokeo ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi wanafunzi wote walifaulu kwa wastani wa A na B tu. Hivyo walifaulu kwa asilimia 100%.," alisema Massesa.  

Alisema kwa Shule ya Sekondari Eckernforde Cambridge mwaka huu imeshika nafasi ya 13 kati ya shule 312 Mkoa wa Tanga katika mtihani wa MOCK-MKOA. na kwa upande wa mtihani wa taifa mwaka 2025 wanafunzi wote walifaulu kwa aslimia 100%.

Alisema wakati wanaadhimisha miaka 27 toka shule shule ya Msingi ilipoanzishwa na miaka 20 toka Shule ya Sekondari ilipoanzishwa, hakika wanajivunia kwa umri huo walioufikia.

“Sifa, utukufu na Shukrani ni kwa Mwenyezi Mungu kwa kumtumia Mkurugenzi Mwanzilishi Hayati Remency Tarimo kwa kuanzisha Shule hizi,” alisema Mwalimu Massesa.

     CHANGAMOTO

Alitaja baadhi ya changamoto ni muamko mdogo kwa baadhi ya wazazi/walezi kufuatilia maendeleo ya watoto wao Shuleni.

Baadhi ya wanafunzi wa kutwa kuto hudhuria Shuleni siku zote za wiki, hii inasababisha kurudisha nyuma wastani wa matokeo ya mitihani ya kimadarasa na pia wanarudisha nyuma juhudi za walimu.   

Alitaja changamoto nyingine ni baadhi ya wazazi kutokukamilisha kulipa Ada ya Shule na michango mbalimbali kwa wakati. 

Mwalimu Massesa alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wanafunzi wote wanaohitimu kwa kuonesha bidii, uvumilivu na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chao chote cha masomo yao.

Alisema mafanikio hayo yametokana na juhudi zao binafsi, majitoleo na ushirikiano wa walimu pamoja na msaada mkubwa wa wazazi na walezi wao.

Mwalimu Massesa aliwaambia wahitimu hao kukumbuka kuwa kuhitimu kwao siyo  mwisho wa safari ya masomo yao bali ni mwanzo wa hatua mpya ya maisha yao.

“ Endeleeni kuwa na nidhamu njema, uadilifu, uzalendo wa kweli, kaipendeni na muikumbatie haki na bidii ikatawale katika kila mtakalofanya,” alisema Mwalimu Massesa.

Mwalimu Massesa aliwaambia kuwa Kamwe wasikubali kushawishiwa na makundi mabaya yenye nia ovu na ubinaadamu wao na taifa letu, wajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya, vitendo vya ukatili au tabia zinazoweza kuharibu maisha yao.

“ Tumieni elimu mliyoipata kutatua changamoto za jamii na ikawe chachu ya kujiletea maendeleo na kufanikisha ndoto kubwa mlizonazo, katu msikubali kuwa chanzo cha kuongeza changamoto katika jamii yetu,” alisema Mwalimu Massesa.
Wanafunzi wa Skauti Alice Abel na Amina Iddi wakimvika Skafu mgeni rasmi wa mahafali hayo.

Mwanafunzi wa Shule ya Awali ya Eckernforde, akimuonesha umahiri wa masomo aliyofundishwa, mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo pamoja na Mkurugenzi wa shule hiyo Sir Omary  Mbogo.


Mtendaji Mkuu wa wa mtandao wa wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali nchini Tanzania (TAMONGSCO), Benjamin Nkonya akitoa salamu za mtandao huo.
Mtendaji Mkuu wa wa mtandao wa wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya serikali nchini Tanzania (TAMONGSCO), Benjamin Nkonya akimpongeza Mkurugenzi wa shule hizo, Sir. Omary Mbogo kwa maboresho makubwa ya shule hizo.

Mkurugenzi wa shule hizo Sir. Omary Mbogo, akiwasalimia washiriki wa mahafali hayo.
Mkurugenzi wa shule hizo, Sir. Omary Mbogo akiteta jambo na  Mkuu wa Shule ya Eckernforde English Medium Nursery and Primary School, Yohana James.
Mwanafunzi Mhitimu wa Kidato cha nne, Adam Hamadi, akimkabidhi picha Mkurugenzi wa shule hizo Sir. Omary Mbogo aliyoichora.
Viongozi wakionesha furaha wakati wa mahafali hayo.
Mkuu wa Sekondari yaa Eckernforde, Salum Massesa, akitoa historia ya shule hiyo.

Mkuu wa shule ya Eckernforder English Medium Nursery and Primary School, Yohana James, akizungumza.

Viongozi wakiwa jukwaa kuu katika mahafali hayo.Ndugu wa Mwanzilishi wa Shule hizo, wakisalimia wageni waalikwa.Viongozi wakiwa meza kuu.Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa ugawaji wa vyeti kwa wahitimu..Mwanafunzi Diana Emmanuel akimuelekeza mgeni rasmi stadi za masomo kwa vitendo alipotembelea mabanda mbalimbali wakati wa mahafali hayo.Mhitimu wa kidato cha nne, Gift Benjamin Mdoe akipongezwa na ndugu, jamaa na wazazi wake.Mhitimu wa kidato cha nne, Gift Benjamin Mdoe akipongezwa na Baba yake.Mhitimu Bakari Is-haka aliyefanya vizuri akikabidhiwa cheti.Mhitimu aliyefanya vizuri, Ebigael Stanley akikabidhiwa cheti.Mhitimu Ebigael Stanley akiwa na wazazi wake wakionesha furaha zao.Wanafunzi wa Shule ya Awali wakionesha vyeti vyao

Mtoto wa Shule ya Awali akikabidhiwa cheti
Mshereheshaji (MC) Mwalimu Said Thabiti akiwajibika ipasavyo kwenye mahafali hayo
Mwanafunzi Agness Daniel akionesha vazi la Utamaduni wa kabila la Kimasai wakati wa maonesho ya mavazi mbalimbali.
Wanafunzi hao wakionesha vazi la wahudumu wa Ndege.
Wakionesha vazi la Waislamu.
Wakionesha vazi la Wakrito wanapo kwenda kanisani.
Wakionesha mavazi ya kutokea watoto.
Wakionesha mavazi wanayovaa wanafunzi baada ya muda wa masomo.
Wakionesha mavazi ya shuleni.
Mhitimu, Bakari Is-haka akigani utenzi.
Washereheshaji (MC) wa mahafali hayo, Mwalimu Saidi Thabiti na Daffa Mhina (kulia), wakiwajibika ipasavyo 'Hadi Raha'
Burudani ya shoo ya muziki ikitolewa.
Burudani ikiendelea.
Mpiga Gitaa la Solo wa Bendi ya Shule hiyo, John Paul akiwajibika.
Mpiga kinanda wa bendi hiyo ya shule, Christina Sisile akikonga nyoyo za wadau wa muziki.
Wanamuziki wa Bendi ya Shule hiyo wakiwajibika ipasavyo jukwaani.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio mbalimbali katika mahafali hayo.
Matukio yakichukuliwa na wapiga  piga picha wanafunzi.
Mahafali yakiendelea.

Mwanafunzi wa Shule hiyo Khalfan Saidi akionesha kipaji chake cha utangazi na kufanya mahojiano na wanafunzi wenzake kwa umahiri mkubwa kwa lugha ya kiingereza 'Hongera walimu kwa kazi nzuri'



Burudani ikiendelea.
Burudani ikitolewa.
Mpiga kinanda wa bendi ya shule hiyo, Glory Mdoligo wa kidato cha kwanza akitoa burudani safi kwenye mahafali hayo.
Wapiga gitaa wa shule hiyo, Charles Chalamila na Brian Tesha wakifanya yao kwenye mahafali hayo.
Walimu na wafanya kazi wa shule hiyo wakiwa kwenye vazi maalumu kwenye mahafali hayo.
Burudani ikiendelea
Wahitimu wa darasa la saba wakitoa burudani yenye ujumbe wa kitaaluma kwenye mahafali hayo.

Wanafunzi wa Shule ya Awali wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wazazi na ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye mahafali hayo.
Burudani ikiendelea.
Burudani ikitolewa.
Nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wa kitaalumu zikiimbwa.
Watoto wa Shule ya Awali wakitoa burudani.
Burudaani ikiendelea.

Mshereheshaaaji (MC) Mwalimu Said Thabiti, akiwajibika zaidi ya uwajibikaji 'Big Up sana Mwalimu'

MC Daffa Mhina akitawala mahafali hayo kwa kazi iliyotukuka.
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa katika ubora wao kwenye mahafali hayo.

Burudani ikiendelea.
Burdani ikiendelea.

Wanafunzi wa shule ya Awali wakiwajibika ipasavyo 'Hongereni walimu kwa malezi ya watoto hawa'
Mahafali yakiendelea
Skauti wakiimba wimbo wa Taifa
Wafanyakazi na walimu wa shule hiyo wakishiriki kuimba wimbo wa Taifa "Hakika mmependeza sana'
Picha zikipigwa.
Skauti wakimuongoza mgeni rasmi eneo lilipo jukwaa kuu.
Wanafunzi wabunifu wa gari wakiwa kwenye banda lao. Kutoka kushoto ni Hassan Hamisi, Paul Sima mbunifu kiongozi wa gari hilo) na Dastan Bongola. Watoto wa shule ya Awali wakiwa kwenye mahafali hayoWanafunzi wa Shule ya Awali wakionesha vyeti vyao.

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.

No comments:

Post a Comment