1. KUDHIBITI Mwendokasi (Speed) kwa kuweka alama za mwendo kikomo maeneo yenye halaiki, kama vile sokoni, mashuleni, na mijini; na kuweka tafsiri sahihi ya maana ya maeneo ya makazi.
2. Kuwafanya wote dereva na abiria wa Pikipiki avae Kofia ngumu (helmet), ili abiria asiyevaa kofia na ipo apigwe faini yeye mwenyewe;
3. Kuwafanya abiria wote kwenye gari wafunge mikanda (seat belts) na sio wa siti za mbele tu. Kwani ajali zinapotokea abiria wote wanapata madhara. Sheria itamke wazi kuwa abiria asiyefunga mkanda atawajibika kulipa faini;
4. Kufanya kiwango cha pombe (alcohol) kilichotajwa kwenye sheria hivi cha 0.08g/dl ni kikubwa mno kulingana na viwango vya kimataifa, sasa kipungue hadi kufikia 0.05g/dl.
5. Kufanya magari madogo yanayobeba watoto kuwa na vizuizi vya watoto (child restraint) au siti za watoto ili waweza kuwa salama inapotokea ajali.
Hili ni eneo la kwanza la kipaumbele linaloangaliwa katika mabadilko ya sheria ya usalama barabarani ili kukabiliana na vihatarishi vitano (5 risk factors) vilivyoainishwa hapo juu. Vipaumbele hivi vimeanishwa na Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kupunguza ajali (UN Decade of Action) na nyaraka mbalimbali za kimataifa ikiwemo za Shirika la Afya Duniani (WHO).
Mabadilliko mengine makubwa (comprehensive amendments) yanatakiwa pia kutokana na baadhi ya vifungu na vipengele vya sheria ya sasa ya usalama Barabarani kupitwa na wakati.
Kwa mfano, kifungu cha 56 hakisemi kuendesha taratibu sana (driving unreasonably slow) ni speed ngapi? Aidha, sheria hadi sasa inalazimisha magari ya abiria, ya mizigo na yaliyobeba milipuko tu kusimama kwa lazima kwenye kivuko cha reli. Ina maana magari madogo hayalazimishwi, nk.
Hayo ni maeneo machache tu yanayohitaji mabadiliko. Tutaendelea kuwaletea maeneo mengine zaidi.
RSAadmin1
RSA TANZANIA
Tunataka Mabadiliko ya Sheria
No comments:
Post a Comment