ASKOFU GWAJIMA ALIVYOWAVUNJA MBAVU RAIS MAGUFULI, SPIKA NDUGAI NA WABUNGE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 16 November 2020

ASKOFU GWAJIMA ALIVYOWAVUNJA MBAVU RAIS MAGUFULI, SPIKA NDUGAI NA WABUNGE

Spika Job Ndugai na Rais Dk. John Magufuli wakicheka bungeni.

MBUNGE mpya wa Jimbo la Kawe, Dar es Salaam, Askofu Josephat Gwajima ‘aliwavunja mbavu’ Rais  Dk. John Magufuli, Spika Job Ndugai, viongozi wengine wakuu, wabunge na wageni waalikwa  alipotoa neo la utani kwa watani wao Wasukuma, Wagogo kuwa enzi hizo Baba wa Taifa, Julius Nyerere aliwaambia Wagogo wapanue mashamba yao ili yawe makubwa wapate mazao mengi, lakini wao hawakumuelewa, badala ya kupanua mashamba wao wakapanua masikio.

Hiyo ilionekana kama ni majibu ya utani aliousema Spika Ndugai  bungeni mwishoni mwa wiki kuwatania watani wao Wasukuma kuwa wameingia jijini Dodoma, hivyo kwa’ ushamba wao’ wawe wanangalia vizuri barabrani wasije wakagongwa na magari. Gwajima ni msukuma na Ndugai ni Mgogo hivyo utani kwao ni kitu cha kawaida.Tukio hilo la aina yake la kuchekesha lilitokea wakati Spika Ndugai alipompatia fursa Askofu Gwajima kutoa neo la shukrani kwa niaba ya wabunge baada ya Rais Magufuli kulifungua rasmi Bunge la 12 Novemba 13, 2020.

No comments:

Post a Comment