Mmoja wa washiriki kwenye Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible' akijadili jambo katika kongamano hilo lililofanyika jana kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam. |
Sehemu ya akinamama wajasiliamali na wageni mbalimbali wakifuatilia mijadala kwenye Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible' jana kwenye Hotel ya Serena Dar es Salaam. |
Na Joachim Mushi, Dar
AKINAMAMA Wajasiriamali mbalimbali wamekutana katika
kongamano la 'Woman of Influence, I'm Possible' kujadili changamoto za ugonjwa
wa Covid 19 nchini kwenye shughuli zao na kujadiliana namna ya kujikwamua na
changamoto hizo. Kongamano hilo lililoratibiwa na Mkurugenzi wa The East Africa
Bang! Magazine, Bi. Emelda Mwamanga limefanyika jana kwenye Hotel ya Serena
jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanawake wajasiliamali na wageni
mbalimbali ambapo mijadala na mada anuai ziliwasilishwa kuwajengea uwezo
akinamama hao.
Akizungumza na wanahabari katika kongamano hilo, Bi. Emelda
Mwamanga alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha akinamama na kujadili
changamoto zilizojitokeza, kushirikishana namna ya kukabiliana nazo na
kuwajengea uwezo jamii hiyo kuweza kufanya vizuri zaidi kwenye shughuli zao kwa
mwaka ujao wa 2021. Alisema sehemu kubwa ya biashara zikiwemo za kinamama
ziliathirika kiasi kikubwa na ujio wa janga la corona, hivyo kuna kila sababu
ya kuyajengea uwezo makundi mbalimbali wakiwemo akinamama wajasiriamali kuweza
kukabiliana na janga hilo.
Alisema Bang Magazine wamekuwa chachu ya kutamani maendeleo
ya akinamama ndio maana wamekuwa wakiwakutanisha kila mwaka tangu 2004, kusudi
kubwa ikiwa ni kumjengea uwezo mwanamke kwa kuwakutanisha na wenzao
waliofanikiwa zaidi ili waweze kuwasaidia wenzao kujikwamua zaidi kimafanikio.
Naye Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya ZARA Tours,
Bi. Zainab Ansell akizungumza kwenye Kongamano hilo, alisema wao kama
wajasiriamali wanawake waliopo katika sekta ya utalii wamejipanga kuhamasisha
utalii wa ndani ili kuziba pengo la upungufu wa watalii kutoka nje lililotokana
na janga la corona.
"...Sisi toka sekta ya utalii tumeanza kuhamasisha
utalii wa ndani kwa kuhamasisha jamii kuanza kutembelea sehemu zetu mbalimbali
za vivutio vya utalii, tayari tumefanya hivyo hapo nyumba na sasa tunaandaa
mapumziko ya mwezi Desemba, Siku Kuu ya Krismas wengine waweze kutembelea mbuga
zetu anuai na hata kupanda Mlima wa Kilimanjaro," Bi. Zainab Ansell.
Alisema Tanzania ina sehemu nzuri na za kujivunia za utalii
hivyo Watanzania wanatakiwa kuelimishwa na kuhamasishwa kuzitembelea;
"Ukiangalia hata tozo za kutembelea mbuga zetu kwa Watanzania zipo chini
sana ukilinganisha na za wageni kutoka nje ya nchi...kinachotakiwa ni
kuelielimishwa na kuhamasishwa wao kutembelea rasilimali hizo za taifa,"
alisema. Aliongeza kuwa kampuni ya ZARA ina tozo maalum kwa Watanzania
watakapenda kutembelea sehemu mbalimbali za vivutio vya utalii ikiwa ni
kuchochea utalii wa ndani kwa jamii ya Watanzania.
Kwa upande wake, Mjasiliamali toka sekta ya utalii, Bi.
Leina Lemomo amesema wameanzisha ushawishi wa tozo maalum za kiafrika (African
rates) maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchochea utalii wa ndani. Amesema
ndoto zao ni kuona kunakuwa na tozo maalum kwa Waafrika wanapotembelea nchi na
maeneo mbalimbali ya bara la Afrika.
"Ndoto yetu ni kuona kwamba kunakuwa na tozo maalum kwa ajili ya waafrika tunapotembelea sehemu mbalimbali ndani ya Bara la Afrika, tunataka ukisafiri kiutalii hata kwenye ndege kuwepo na punguzo la malipo maalum kwa waafrika, vivyo hivyo kwenye hoteli mbalimbali barani Afrika...hii inawezekana na inaweza pia kuchochea utalii wa ndani kwa Waafrika. Ukienda mabara mengine tozo kama hizo zipo kwa raia wao na sisi hili kuna haja ya kulipigia debe sote kwa pamoja," alisema Bi. Lemomo.
Mjasiliamali Bi. Leina Lemomo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye 'Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible'. |
Sehemu ya akinamama wajasiliamali na wageni mbalimbali wakifuatilia mijadala kwenye Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible' jana kwenye Hotel ya Serena Dar es Salaam. |
Sehemu ya akinamama wajasiliamali na wageni mbalimbali wakifuatilia mijadala kwenye Kongamano la Woman of Influence, I'm Possible' jana kwenye Hotel ya Serena Dar es Salaam. |
Sehemu ya maonesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea katika kongamano hilo. |
Sehemu ya maonesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea katika kongamano hilo. |
Sehemu ya washiriki wakiwa katika banda la Bang! Magazine kwenye kongamano hilo. |
Sehemu ya maonesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea katika kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment