NMB YAKABIDHI MISAADA YA MIL. 21.6/- SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI MALINYI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 21 February 2026

NMB YAKABIDHI MISAADA YA MIL. 21.6/- SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI MALINYI

 

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba (wa tatu kushoto) akikabidhiwa mmoja ya meza 100 na Meneja wa benki ya NMB kanda ya kati, Janeth Shango (wa pili kulia) katika hafla ya benki hiyo ya kukabidhi vifaa vya shule wilaya ya Malinyi vyenye thamani ya sh21.6milioni iliyofanyika katika shule ya sekondari ya Kilosampepo mkoa wa Morogoro. Kulia ni meneja wa Benki ya NMB tawi la Malinyi, Anderson Lyatuu na kuhoto ni wawakilishi wa shule nufaika wa msaada huo.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba (aliyekaa) akifurahia jambo na Meneja wa benki ya NMB kanda ya kati, Janeth Shango pamoja na wanafunzi baada ya Benki hiyo kukabidhi vifaa vya shule vyenye thamani ya sh21.6milioni katika hafla iliyofanyika katika shule ya sekondari ya Kilosampepo mkoa wa Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Sebastian Waryuba akionyesha ishara ya shukrani baada ya benki ya NMB kukabidhi vifaa vya shule kwa wilaya hiyo vyenye thamani ya sh21.6milioni katika hafla iliyofanyika shule ya sekondari ya Kilosampepo mkoa wa Morogoro, wa pili kutoka kulia ni Meneja wa benki ya NMB kanda ya kati, Janeth Shango na wengine ni wanafunzi wa shule hiyo.

KUPITIA  Programu ya Uwekezaji kwa Jamii, Benki ya NMB imekabidhi misaada ya madawati 100, viti 100 na meza 100 kwa shule mbili za msingi na moja ya sekondari wilayani Malinyi, mkoani Morogoro, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 21.6. 

Msaada huo ni sehemu ya Sh. Bil. 7.4 zilizotengwa na benki hiyo kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii katika Sektra za Elimu, Afya na Mazingira kwa mwaka 2026, ikiwa ni asilimia moja ya Faida Baada ya Kodi ya Mwaka wa Fedha ulioishia Desemba 31, 2025. 

Meneja wa NMB, Kanda ya Kati, Bi. Janeth Shango, ndiye aliyekabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mhe. Sebastian Waryuba, aliyeipokea kwa niaba ya walimu wakuu wa Shule za Msingi Madibila Chini, Salamiti na Shule ya Sekondari Kilosa Mpepo, zote za Malinyi.  

Akizungumza katika hafla iliyofanyika shule ya sekondari Kilosa Mpepo, Bi. Shango alisema Shule ya Madibila Chini imepewa madawati 50, idadi sawa na waliyopewa Shule ya Msingi Salamiti, huku Shule ya Sekondari ya Kilosa Mpepo ikisaidiwa viti 100 na meza 100 kwa ajili ya wanafunzi. 

Msaada huu ni uthibitisho wa ushiriki wa Benki ya NMB katika maendeleo ya kijamii na kurejesha kwa jamii kutokana na faida walioipata. Na ni kupitia michango hii, Benki ya NMB imeweza kusaidia katika mbadiliko kwenye sekta ya elimu na pia kuifanya kutwa tuzo ya Benki Kinara wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Jarida la Global Banking and Magazine la Marekani.

Kwa upande wake, DC Waryuba, aliishukuru na Kuipongeza Benki ya NMB kwa msaada huu wenye thamani ya Sh. Mil. 21.6. huku akibainisha kuwa kwa hesabu za haraka haraka utagundua kuwa kupitia madawati, viti na meza hizi, zinaenda kuwatoa sakafuni watoto takribani 500 wa shule hizi waliokuwa wakisoma chini.

DC Waryuba aliongeza kuwa tayari NMB imefungua njia katika kuboresha elimu wilayani Malinyi na kuwataka wadau zaidi kufuata nyayo za benki hiyo kwa kujitolea kusaidia, huku akiwasisitiza walimu na wanafunzi umuhimu wa kutunza misaada hiyo ili kuwatia moyo wafadhili hao.

 

__________. _________. __________. __________. ___________

 

NMB handed over Tsh 21.6 million in donations to primary and secondary schools in Malinyi

Through its Corporate Social Investment Program, NMB Bank has donated 100 desks, 100 chairs and 100 tables to two primary schools and one secondary school in Malinyi district, Morogoro region, worth a total of TSh 21.6 million.

This donation is part of Tsh 7.4 billion the bank set aside to support community projects in the Education, Health and Environment sectors for 2026, equivalent to one percent of the Profit After Tax for the fiscal year ended December 31, 2025.

NMB Bank’s Central Zone Manager, Ms. Janeth Shango, handed over the donations to the Malinyi District Commissioner, Hon. Sebastian Waryuba, who received them on behalf of the headteachers of Madibila Chini Primary School, Salamiti Primary School and Kilosa Mpepo Secondary School, all in Malinyi.

Speaking at the event held at Kilosa Mpepo Secondary School, Ms. Shango said Madibila Chini Primary School received 50 desks, the same number was given to Salamiti Primary School, while Kilosa Mpepo Secondary School received 100 chairs and 100 tables for students.

This support demonstrates the Bank’s participation in social development and returning value to the community from its profits. Through such contributions, NMB Bank has helped bring change in the education sector and has earned recognition, including being awarded Best Bank in Corporate Social Responsibility by Global Banking Magazine (USA).

DC Waryuba thanked and commended NMB Bank for the Tsh 21.6 million contributions, noting that a quick calculation shows that these desks, chairs and tables will lift nearly 500 pupils who had been studying on the floor.

DC Waryuba added that NMB has already opened a path to improving education in Malinyi and urged more stakeholders to follow the bank’s example by voluntarily supporting; he also stressed to teachers and students the importance of taking care of the donated items to encourage further donors.

No comments:

Post a Comment