Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akionesha mfano wa hudi hizo juu mara baada za kukabidhiwa.
WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameziagiza hospitali zote za rufaa ambazo zinatoa matibabu ya ugonjwa wa saratani kwa watoto kuangalia uwezekano wa kuwa na wodi maalum kwa ajili ya wagonjwa hao. Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipokea mfano wa hudi ya shilingi milioni 100 zilizochangwa na wakimbiaji wa NMB Bima Marathon, fedha zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia matibabu ya ugonjwa wa saratani kwa watoto kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili. Akikabidhi hundi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin P. Mhede, pamoja naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ambao ni waratibu wa mbio hizo, alisema wameguswa na kundi hilo la wagonjwa wa saratani ambao wanaitaji msaada hivyo kuamua kuwasaidia kwa kiasi kilichopatikana. Baada za Waziri Mkuu Majaliwa kukabidhiwa hundi hizo, alimkabidhi rasmi moja kwa moja Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru ambapo alieleza kuwa gharama kubwa za matibabu za ugonjwa wa saratani imekuwa kikwayo kwa jamii hivyo wanafarijika michango na misaada inazotolewa kusaidia matibabu hazo. Mbio za NMB Bima Marathon zilizofanyika leo jijini Dar es Salaam zimeshirikisha wakimbiaji mbalimbali wa kuanzia kilomita 5, 10, 20 ambapo zimekuwa na muitikio mkubwa wa washiriki kutoka makampuni anuai, ambapo washindi walikabidhiwa medali na fedha.
|
No comments:
Post a Comment