Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli. |
RAIS wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ametangaza kuzifungua shule zote nchini zilizofungwa kwa sababu ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona nchini. Rais Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akilihutubia Bunge la Tanzania kabla ya kulivunja rasmi, kuashiria kuanza rasmi shughuli za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020.
Rais Magufuli amesema shule zote zitafunguliwa rasmi tarehe 29, mwezi Juni pamoja na shughuli zingine zote ambazo zilisimamishwa awali kwa ajili ya kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona nchini.
No comments:
Post a Comment