Marehemu Abdukarim Shah. |
MBUNGE mstaafu wa Mafia Mh. Abdukarim Shah amefariki dunia katika hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam. Taarifa zinasema mwili wa marehemu Shah upo Hospitalini Hindu Mandal ukisubiri taratibu za mazishi ambayo yatafanyika katika makaburi ya Kisutu. Msiba upo Ilala karibu na geti la Amana Hospital.
Wakati huo huo, uongozi wa kamati ya Ustawi ya RSA TANZANIA Umesikitika kwa kifo cha Balozi Abdulkareem Shah. Katika Uhai wake, Shah aliwahi kuwa mwanachama wa RSA TANZANIA na Mjumbe wa Bodi wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani pia Alishawahi kuwa mbunge wa Mafia, Chief Kamishna wa Scouts Association.
No comments:
Post a Comment