KENYA YAONGEZA MARUFUKU YA KUTOTEMBEA KWA SIKU 21...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 26 April 2020

KENYA YAONGEZA MARUFUKU YA KUTOTEMBEA KWA SIKU 21...!

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameongeza muda wa marufuku ya watu kusafiri na kuingia au kutoka katika Jiji la Nairobi na miji mingine minne kwa muda wa siku 21. Bwana Kenyatta pia ameongeza tena muda wa amri ya kutotoka nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri kwa siku 21 zaidi.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza marufuku ya kuingia na kutoka katika kaunti za Nairobi, Kilifi, kwale Mombasa huku taifa hilo sasa lina maambukizi mapya ya wgonjwa saba na kufanya Kenya kuwa na visa 343 na wagonjwa waliopona ni 98.

Marufuku hii imetangazwa baada ya ile iliyotolewa siku 21 zilizopita kwa lengo la kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona. Rais huyo wa Kenya amepuuzia mbali madai kuwa Wakenya watatumiwa na wanasayansi wa nchi za kigeni kufanyiwa majaribio ya chanjo ya corona.

''Watafiti wetu katika vituo vya utafiti vya Kenya wanashirikiana na wanasayansi wengine katika kutafuta chanjo, kama ijtafika wakati watatuambia kuwa majaribio yatahitaji kufanywa kwa binadamu basi tutawafahamisha kama ambavyo tumekua tukiwaeleza'', alisema,Bwana Kenyatta.

Japo amesema kuwa kumekua na mafanikio katika juhudi za kudhibiti ugonjwa, ingawa bado baadhi ya watu hawajaweza kuzingatia ushauri unaotolewa ili kuzuia maambukizi.

Wakati huohuo amesema hatua zaidi zitachukuliwa kuhusu kaunti za Mandera, Kilif, Kwale na Mombasa kwa ushauriano na magavana wa kaunti hizo. Hivi karibuni idadi ya maambukizi imekua ikiendelea kuongezeka katika katika kaunti ya Mombasa.

Akizungumzia jukuhusu hatua za kukabiliana na athari za janga la corona Bwana Kenyatta amesema Jumatano serikali itaanzisha awamu ya kwanza ya mipango ya kitaifa ya usafi ambayo amesema itasaidia kutoa ajira hususan kwa vijana. Mipango hiyo inatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 26,000 na baadae awamu nyingine za mipango hiyo zitaendelea na kutoa ajira zaidi.

Amesema uwezeshaji wa shilingi bilioni 8 tayari umekwishaanza kutolewa kwa ajili ya kuwasaidia raia wanaoishi walio katika hatari zaidi ya kupata maambukizi hususan katika makazi duni katika kaunti 7 zilizoathiriwa zaidi. Hatua ambazo Kenya zinafuatazo kukabiliana na maambukizi ya corona; Kuvaa barakoa kila mara wanapokua katika maeneo ya umma. Kunawa mikono kwa sabuni.

Kuendelea kuepuka kukaribiana na kuzingatia ushauri wa kukaa mita mbili kutoka kwa mtu mwingine. Wasiwaweke hatarini watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 na wenye magonjwa ya kudumu. Amewataka mafundi wa nguo kutengeneza barakoa nyingi na akasema maafisa wa afya watawaelekeza namna zinavyotengenezwa.

Gari lolote la mizigo halitaruhusiwa kuwa na watu zaidi ya watatu na inapaswa kuwa na kibali cha maafisa. Usafirishaji wa chakula utaendelea kama kawaida. Wizara ya afya nchini humo ilitangaza wazi kuwa kwamba inatengeneza barakoa ambazo zitasambazwa kwa wananchi hivi karibuni.

Wizara ya afya imeeleza kuwa watu watakaokufa kutokana na virusi vya Corona watazikwa ndani ya saa 24 huku watu wa karibu wa familia wasiozidi 15 wakiruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayoandaliwa na Serikali.

Aidha, ndege kutoka nchi za kigeni zimeendelea kipigwa marufuku kuingia Kenya kwa siku 30 zaidi.
Hata hivyo, marufuku hii iliondolewa kwa ndege za kigeni zinazokuja kuhamisha raia wa nchi za nje waliokwama ingawa zinatakiwa kutoa taarifa kwa serikali angalau saa 72 kabla.

Ndege zingine ambazo hazitaathirika na marufuku hii ni zile za kubeba mizogo hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa serikali inaagiza vifaa vya wahudumu wa afya kutoka nje.

Na kutokana na ongezeko hilo, kuanzia Jumatatu, matatu au daladala pamoja na bodaboda ambazo zitakiuka sheria zilizowekwa zitapokonywa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kusambaza virusi kimaksudi.
-BBC

No comments:

Post a Comment