DC wa Mtwara, Evod Mmanda. |
MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amefariki dunia alfajiri ya leo Jumatatu, Aprili 27, 2020 katika Hospitali ya Ligula, Mtwara kutokana na maradhi ya moyo. Mmanda ambaye kitaaluma ni mwanasheria mkongwe aliteuliwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa DC wa Mtwara, Desemba 2016. Aliwahi pia kuwa kiongozi wa Chama cha NCCR-Mageuzi mwaka 2005 kabla ya kurejea CCM.
No comments:
Post a Comment