TANZIA : DK. MAKONGORO MAHANGA AFARIKI DUNIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 23 March 2020

TANZIA : DK. MAKONGORO MAHANGA AFARIKI DUNIA

Milton Makongoro Mahanga.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya kiongozi na mwanachama wao maarufu, Milton Makongoro Mahanga kufariki dunia leo. Taarifa iliyotolewa na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Ilala, Jerome Olomi imesema; "taarifa mbaya tusizozitegemea tulizozipata asubuhi hii Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ilala Dr. Milton Makongoro Mahanga amefariki dunia.

Akifafanua zaidi Katibu huyo alisema wataendelea kutoa taarifa za taratibu nyingine wakati wakiendelea kufanya mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki.

No comments:

Post a Comment