POLISI YA RWANDA INASEMA MSANII MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI KIZITO MIHIGO AMEJINYONGA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 17 February 2020

POLISI YA RWANDA INASEMA MSANII MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI KIZITO MIHIGO AMEJINYONGA


Mwanamuziki maarufu kwa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo

Polisi ya Rwanda imetangaza kwamba msanii maarufu wa nyimbo za injili, Kizito Mihigo ''amejinyonga'' Polisi wa Rwanda wanasema.

Kwa mujibu wa tangazo la polisi, maiti ya msanii huyo imepatikana katika chumba alimokuwa anazuiliwa kwenye kituo cha polisi mtaa wa Remera, mjini Kigali.

Polisi imesema kwamba amejinyonga siku tatu baada ya kukamatwa karibu na mpaka baina ya Rwanda na Burundi katika kile ambacho polisi ilisema alikuwa na nia ya kutoroka nchi na kujiunga na makundi ya waasi dhidi ya Rwanda.

Alikuwa ameanza kufanyiwa uchunguzi kuhusu madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkataa.

Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha raia kupinga serikali.



Mwaka 2015, Bwana Kizito alikutwa na hatia kwa kosa la jaribio la kutaka kumuua Rais Paul Kagame na kuhamasisha vurugu dhidi ya serikali na kufungwa lakini baadae alisamehewa
Kumekuwa na hisia mseto katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha ghafla cha msanii huyo wa muziki wa injili huku baadhi ya watu wakitaka majibu kutoka kwa serikali.

Kizito, aliyekuwa na miaka 38 alipata umaarufu kutokana na nyiimbo zake kama vile 'Inuma' unaomaanisha njiwa na 'Igisobanuri cy'urupfu' ambao unaelezea kifo ni nini.

-BBC

No comments:

Post a Comment