Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
ONGEZEKO la idadi ya wanafunzi wanaokatishwa masomo kwa kupewa mimba limeibua hofu kwa wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi,Ambao baadhi yao wameshindwa kuvumilia na kuamua kuungana na serikali kusaidia kukabiliana na tatizo hilo
La Mimba kwa wanafunzi wakike.
Na Miongoni wa wadau hao kutoka nje ya nchi ni pamoja na wahisani Kutoka Nchi ya Korea ambao wamejitolea kusaidia nakwa Upande wa wadau wa ndani ni pamoja na Taasisi ya Kifedha ya Benk ya Exim ambayo imetoa milioni 25 kwa ajili kutengeneza vitanda ikiwa ni mchango wao kusaidia kuwawezesha wanafunzi kulala shuleni
Akipokea misaada hiyo Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewashukuru wahisni hao kwa hatua hiyo kubwa huku akiwataka wengine kuiga mfano huo ambao umeongeza nguvu katika jitihada za serikali za kutekeleza mkakati wake wa kuimarisha upatikanaji wa mabweni mashuleni ambao ni sehemu ya suluhisho la tatizo la mimba kwa wanafunzi hasa wanaotembea umbali mrefu kwenda na kurudi ambao wamekuwa wakikabliliwa na changamoto nyingi njiani.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Kifedha ya Exim kutoka makao makuu Dar es salam Bw Jafari Matundu amesema msaada waliotoa ni sehemu ya kuchangia sekta ya Elimu na wataendelea kushirikiana na wadau wengine kusaidia miradi ya maendeleo ya wananchi
Uku shirika la Maendeleo la Korea Koika nalo limetoa wataalam 10 wa kujitolea kuwaelimisha wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari juu ya Masomo ya Tehama na sayansi kuwasaidia katika Maisha na masomo yao ambayo yameanzia kwenye shue ya sekondari ya Mrisho Gambo iliyoko Kata ya Olasiti .
Hata hivyo viongozi wa mkoa wa Arusha wamepokea mashine moja ya kisasa ya kutolea nakala iliyotolewa na baadhi ya wadau yenye thamani ya milioni 11 ambayo inatarajiwa kusaidia kufanikisha mkakati wa mkoa wa Arusha wa kuandaa Mitihani ya majaribio kwa wanafunzi inayofanywa na shule zote za mkoa wa Arusha .
Pamoja na mkoa wa Arusha kuwa miongoni mwa mikoa kumi bora katika ufaulu kitaifa bado unakabiliwa na tatizo kubwa la wanafunzi kukatishwa masomo kwa ajili ya mimba sababu zinazotajwa wengi wao kusoma shule zakutwa ambazo hulazimika kutembea umbali mrefu kwenda shule.
No comments:
Post a Comment