RAIS MAGUFULI AONGOZA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA BOEING 787-8 DREAMLINER DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 27 October 2019

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA BOEING 787-8 DREAMLINER DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine na wadau akikata utepe kuashiria kupokewa kwa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo wakisiliza maelezo toka kwa Kepteni Dennis Mshana mmoja wa Marubani walioileta ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Seattle Marekani hadi katika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuaga baada ya kuongoza mamia ya  wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama alipoongoza wananchi katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kiti cha rubani  Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea katika Uwanja  wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019.

Mke wa Rais Mama janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakifurahia jambo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuipokea ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner katika Uwanja  wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Oktoba 26, 2019.

No comments:

Post a Comment