WIZARA ya mawasiliano na vyombo vya habari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imethibitisha kuwa mabaki ya ndege iliyopotea juma lililopita ikiwa imebeba gari la raisi wa nchi hiyo Felix Tshisekedi yamepatikana jimboni Sankuru katikati mwa nchi hiyo.
Awali palikua na taarifa kinzani kuhusu mahali ndege hiyo ilipo pamoja na idadi ya watu waliokuwemo. Mamlaka imethibitisha kuwa miili ya watu wanne imepatikana huku rubani amethibitishwa kupatikana akiwa hai.
Ndege hiyo ilipotea siku ya Alhamisi ikiwa na watu watano, mmoja wapo akiwa dereva maalumu wa raisi Tshisekedi. Mtoa huduma kutoka taasisi ya kikatoliki alifika eneo la ajali jimbo la Sankuru, huku wanakijiji wakiwa tayari wameshaizika miili ya watu wanne waliopatikana kwenye kifusi.
Kikosi cha wachunguzi kikisaidiana na wataalamu wa Ujumbe wa kulinda amani wa umoja wa mataifa wamefika kwenye aneo la ajali, ofisi ya raisi imesema mpaka sasa sababu ya ajali hiyo haijajulikana.
-BBC
No comments:
Post a Comment