FAMILIA ILIYOJIFICHA CHINI YA ARDHI MIAKA 9 IKISUBIRI MWISHO WA DUNIA....! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 16 October 2019

FAMILIA ILIYOJIFICHA CHINI YA ARDHI MIAKA 9 IKISUBIRI MWISHO WA DUNIA....!

Nyumba hiyo.



FAMILIA moja iliyokuwa ikiishi katika chumba cha chini ya ardhi kwa miaka tisa 'ikisubiri mwisho wa dunia' imepatikana na polisi nchini Uholanzi, ripoti zinasema.

Mwanamume wa miaka 58, na watoto wake sita walio na umri kati ya miaka 16 hadi 25 - walikuwa wakiishi katika shamba lao katika mkoa wa kaskazini wa Drenthe.

Walipatikana baada ya kijana wake mkubwa kuenda kununua pombe katika baa moja karibu na Kijiji cha Ruinerwold, na kumfahamisha mhudumu wa baa hiyo kwamba anataka usaidizi,Kituo cha Televisheni cha RTV kiliripoti.

Waliomuona kijana huyo wanasema alionekana kana kwamba amechanganyikiwa.
Familia yake imekuwa ikiishi kwa kujitenga ikisubiri mwisho wadunia, RTV iliripoti.

"Aliagiza chupa tano za bia na kunywa zote. Baada ya hapo nilisema naye kidogo ndipo alipofichua kuwa ametoroka na kwamba anaomba usaidizi... tukapiga simu polisi," mmiliki wa baa hiyo Chris Westerbeek alikifahamisha kituo cha RTV.

Aliongeza kuwa: "Alikuwa na nywele ndefu, ndevu chafu,nguo zilizochakaa na alionekana kana kwamba amechanganyikiwa. Alisema hajawahi kwenda shule na kwamba hajawahi kunyolewa nywele kwa miaka tisa ."

"Alisema ana ndugu na dada zake ambao wanaishi katika shamba hilo. Pia alisema anataka kukomesha jinsi familia yake inavyoishi."

Maofisa walitembelea makaazi hayo ya vijijini ili kufanya upekuzi zaidi. Waligundua ngazi iliokuwa nyuma ya kabati katika sebule ya nyumba hiyo ambayo inaelekeachumba cha chini ya ardhi ambako familia hiyo ilikuwa ikiishi.

Ruinerwold ni kijiji kilicho na wakazi chini ya 3,000. Shamba hilo lipo nje kidogo ya kijiji hicho na inaweza kufikika tu kupitia daraja lililoko juu ya mfereji.

Shamba hilo ambalo kwa upande mmoja limefichwa na miti mingi pia limepandwa mboga nyingi. Jirani aliviambia vyombo vya habari vya Uholanzi kuwa alimuona mtu huyo peke yake na kwa alifikiria hana watoto.

Watu katika eneo hilo walisambaza taarifa hiyo katika mtandao wa kijamii wa Twitter huku mwanahabari mmoja akiweka picha ya nyumba hiyo na ujumbe kwamba ameambiwa akae mbali na makazi hayo.

Polisi imethibitisha mjini Drenthe imethibitisha kuwa mwanamume huyo wa miaka 58 amekamatwa na kuongeza anafanyiwa uchunguzi-baada ya kukataa kushirikiana nao.
-BBC

No comments:

Post a Comment