RIPOTI ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio
ya Ghasia na Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 2025.
Tukio hili linaashiria mwanzo wa
hatua ya utekelezaji wa mapendekezo ya kuponya Taifa, kuimarisha uwajibikaji na
kujenga mustakabali imara zaidi.
Akizungumza wakati wa kupokea ripoti
hiyo, Mheshimiwa Rais alitambua kwa uzito mkubwa madhara yaliyolikumba Taifa,
akipokea maelezo kuwa matukio hayo yalisababisha vifo vya takribani watu 518,
majeruhi zaidi ya 2,390, na uharibifu wa mali unaokadiriwa kufikia zaidi ya
shilingi bilioni 125.
Alisisitiza kuwa hasara hizi zimeacha
majeraha makubwa ya kijamii, kiuchumi na kisaikolojia kwa wananchi. “Hili ni
janga na doa kubwa kwa Taifa letu.” Alisema Rais Dkt. Samia.
Mheshimiwa Rais alieleza kuwa kazi ya
Tume imeiwezesha nchi kupata uelewa sahihi wa kilichotokea, ikijumuisha
uchambuzi wa kina uliotokana na ushahidi wa mashahidi 1,323, maelezo ya viapo
953, pamoja na maoni yaliyokusanywa kupitia njia mbalimbali ikiwemo zaidi ya
ujumbe mfupi 33,000 na maoni ya maelfu ya wananchi katika maeneo 202
yaliyofanyiwa uchunguzi.
“Wakati mwingine dawa ni chungu,
lakini kama tunataka kupona, lazima tunywe dawa. Tume imechunguza
kilichotusibu. Kazi yetu sasa ni kutumia dawa hiyo ipasavyo,” amesema Rais Dkt.
Samia na kusisitiza kuwa Taifa lina wajibu wa kuhakikisha matukio hayo
hayajirudii kwa kuchukua hatua za marekebisho na uwajibikaji.
Aidha, Mheshimiwa Rais alihimiza
mshikamano wa kitaifa akibainisha kuwa mustakabali wa nchi uko mikononi mwa
Watanzania wenyewe. “Hatma ya Tanzania ipo mikononi mwa Watanzania wenyewe.”
Katika juhudi za kuliponya Taifa, alitoa wito mahsusi kwa viongozi wa dini
kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maridhiano na kurejesha maadili ya
jamii. “Simamieni nafasi yenu ya kuliponya Taifa letu.” Kwa upande wake,
Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, alisema kuwa
Ripoti hiyo ni matokeo ya uchunguzi mpana uliodumu kwa siku 153, ukihusisha
mikoa 11, wilaya 21, na maeneo 202 yaliyoathirika zaidi.
Alieleza kuwa mchakato huo ulihusisha
pia mijadala ya vikundi zaidi ya 200 na ushirikishwaji mpana wa wananchi.
“Ripoti tunayoiwasilisha inabeba dhamira ya pamoja ya Taifa ya kutibu majeraha,
kuwajibika kila panapostahili, lakini muhimu zaidi kujifunza na kusonga mbele,”
alisema Mwenyekiti wa Tume na kuongeza kuwa, licha ya maumivu makubwa
yaliyosikika kutoka kwa waathirika, Watanzania wengi walionesha utayari wa
kushiriki katika safari ya maridhiano na kujenga upya mshikamano wa kitaifa.
“Waliowasiliana na Tume walionesha
wazi kuwa yaliyotokea siyo taswira halisi ya Utanzania wetu.” Mheshimiwa Rais
alikiri uzito wa jukumu lililopo mbele yake na kuahidi kulibeba kwa ujasiri
huku akihimiza ushirikiano wa wote. “Nataka niwahakikishie nitaubeba mzigo huu
kwa ujasiri na kujiamini na hadhari kubwa. Kwa pamoja tutafanya.
Tusimuachie Samia peke yake.” Katika
hitimisho lake, Mheshimiwa Rais aliwataka Watanzania kujifunza kutokana na
yaliyotokea na kusonga mbele kwa umoja na dhamira mpya ya kulijenga Taifa.
“Tumegusa kaa la moto, na tumejifunza,” alisema.
Hii ni Tume ya saba ya Rais ya
Uchunguzi tangu Uhuru. Tume iliundwa tarehe 18 Novemba, 2025 na kuanza kazi
tarehe 20 Novemba, 2025. Tume ilikuwa na wajumbe tisa chini ya uenyekiti wa
Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman. Wajumbe wengine ni pamoja na Prof.
Ibrahim Hamis Juma, Balozi Ombeni Yohana Sefue, Dkt. Stergomena Lawrence Tax,
Bw. Said Ally Mwema, Balozi George Kahema Madafa, Balozi Paul Meela, Balozi
Radhia Naima Msuya na Balozi David Joseph Kapya. 3/3 Tume ilikusanya ushahidi
kutoka kwa maelfu ya wananchi kupitia mbinu mbalimbali za kisayansi na kijamii
ili kubaini ukweli wa matukio na kutoa mapendekezo ya kuimarisha amani,
uwajibikaji na mshikamano wa kitaifa.

.jpeg)



No comments:
Post a Comment